NIYONZIMA AFUNGUKA KUKAA NJE YA UWANJA KUNAVYOWEZA KUMUATHIRI - EDUSPORTSTZ

Latest

NIYONZIMA AFUNGUKA KUKAA NJE YA UWANJA KUNAVYOWEZA KUMUATHIRI







Niyonzima Ahofia Kiwango Chake Kupungua...Hajacheza Mpira Tangu Mwaka Jana November
KIUNGO wa Simba, Mnya­ruanda, Haruna Niyonzima, amefunguka kuwa anahofia kupoteza kiwango chake kuto­kana na kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu.

Niyonzima alipatwa na mata­tizo ya enka na hajacheza mechi yoyote tangu Novemba, mwaka jana, baada ya kuumia mazoezini na kumsababisha kukosa mechi kadhaa za ligi kuu. Yupo nje ya uwanja hadi hivi sasa.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Niyonzima alisema kuwa, anajisikia vibaya kuona anakaa nje kwa muda mrefu huku akikosa mechi za ligi, kwa kuwa mpira ndiyo kazi yake anayoitegemea kwa kuwa kukaa nje kuta­muathiri.

“Kama binad­amu mwingine, siwezi kujisikia vizuri kukaa nje ya kazi yangu kwa muda mrefu, kuta­niathiri mimi, maisha yangu ni mpira, kama sichezi mpira, nitajisikia vibaya zaidi ya una­vyofikiria kwa kuwa sina kazi nyingine zaidi ya mpira ambao ninautegemea.

“Timu yangu inanihitaji niweze kuisaidia na mimi ninahi­taji kuitumikia nisaidie kitu fulani, siwezi ku­furahi nipo nje sichezi mpira, furaha pekee niliyo nayo kwa sasa ni kutokana na kuona timu yangu inafanya vizuri kwenye ligi, lakini kuhusu hali yangu sijisikii vizuri kwa kweli.

“Sijajua bado nitarejea lini uwanjani kwa sababu bado naendelea na matibabu, namuomba Mungu anisaidie,” alisema Niyonzima.

Katika hatua nyingine, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amethibitisha kuwa klabu hiyo itampeleka kiungo huyo nje ya nchi kwa ajili ya matibabu, baada ya kukamilisha taratibu zote ndani ya wiki hii.

Hata hivyo, Manara amesema nchi watakayompeleka kufany­iwa matibabu wataitangaza baadaye.
NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz