'FULL TIME SIMBA 4-0 MAJIMAJI,KUTOKA UWANJA WA TAIFA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 28 January 2018

'FULL TIME SIMBA 4-0 MAJIMAJI,KUTOKA UWANJA WA TAIFA
FULL TIME
Mchezo umemalizika. Simba wanashinda mabao 4-0.
Dk ya 90 + 4: Muda wowote mchezo utamalizika.

Dk ya 90 + 2: Kapombe anachezewa faulo, mwamuzi anapuliza filimbi.
Dk ya 90: Zinaongezwa dakika 4 za nyongeza.
Dk ya 89: Majimaji wanaonekana kukata tamaa.
Dk ya 88: Mavugo anaingia na mpira lakini beki wanatoka, inakuwa kona.
Dk ya 84: Simba wanafanya mabadiliko, Mavugo anaingia anatoka Kichuya.
Dk ya 81: Majimaji wanafika langoni lakini mpira unakuwa offside.
Dk ya 80: Bocco anafika langoni mwa Majimaji shuti lake linapaa juu.
Dk ya 78: Simba imepunguza kasi kiasi.
Dk ya 72: Six wa Majimaji anakosa nafasi ya wazi, anapiga shuti linatoka nje kidogo ya golini.
Dk ya 68: Okwi anafunga bao la nne kwa kumchambua kipa, alipewa pasi na Bocco ambaye aliwachambua walinzi wa Majimaji.
GOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 65:Majimaji wanafanya mabadiliko Jerry Tegete ameingia kuchukua nafasi ya Peter Mapunda
Dk ya 62: Simba wanapata faulo nje ya 18 ya Majimaji, inapigwa inatoka nje.
Dk ya 58: Mchezo umechangamka.
Dk ya 54: Simba wanafanya shambulizi kali, kipa anapangua shuti lingine la Okwi.
Dk ya 52: Okwi anafanya shambulizi lingine kali, kipa anapangua.
Dk ya 50: Emmanuel Okwi anaipatia Simba bao la tatu kwa kichwa, anamalizia mpira wa kona uliopigwa na Kichuya.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 47: Majimaji wanashambulia, Marcel anafanya kazi nzuri lakii mpira unatoka nje.
Simba wanafanya mabadiliko, ametoka Juuko Murshid ameingia Kotei.

Kipindi cha pili kimeanza.
MAPUMZIKO
Mwamuzi anakamilisha kipindi cha kwanza.
Dk ya 45 + 3: Kichuya na Kapombe wanapigiana pasi nzuri.
Dk ya 45+ 1: Majimaji wanafika langoni lakini Manula anakuwa makini kuzuia.
Mwamuzi wa mezani anaonyesha dakika 3 za nyongeza.
Dk ya 45: Simba wanaendelea kutawala mchezo. Majimaji nao wanapambana.
Dk ya 42: Jamal Mwambeleko anatoka anaingia Muzamiru Yasin.
Dk ya 41: Majimaji wanafanya shambulizi kali, shuti linapaa juu.
Dk ya 39: Simba bado wanamiliki mpira muda mwingi.
Dk ya 38: Okwi anapiga shuti kipa wa Majimaji anapangua.
Dk ya 37: Majimaji wanaotea mara ya tano. Mwamuzi anapuliza filimbi.
Dk ya 36: Boniventure anapiga shuti linakuwa na nguvu dogo, Aishi Manula anadaka.
Dk ya 35: Majimaji wanafika langoni mwa Simba lakini Geofrey anakuwa ameotea.
Dk ya 32: Simba wanapata kona.
Dk ya 30: Majimaji wanaonekana kutokuwa makini katika maamuzi yao.
Dk ya 27: Bocco anaipatia Simba bao la pili kwa kichwa, asisti ya Said Ndemla.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 25: Simba wanapata kona, inapigwa inaokolewa.
Dk ya 24: Pasi nzuri ya Kapombe haitumiki vizuri, Bocco anapaisha mpira akiwa yeye na lango.
Dk ya 22: Inapigwa faulo, walinzi wa Simba wanaokoa.
Dk ya 20: Geofrey Mlawa wa Majimaji yupo chini, anapatiwa matibabu karibu ya eneo la 18 la Simba.
Dk ya 16: John Bocco anaipatia Simba bao kwa njia ya kichwa, ilipigwa kona na Kichuya, kukatokea mgongano kisha Bocco akafunga kwa kichwa.
GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO
Dk ya 15: Peter Mapunda wa Majimaji anaingia ndani na mpira lakini walinzi wa Simba wanamuwahi.
Dk ya 11: Simba wanapata kona, anapiga Kichuya inaokolewa.
Dk ya 8: Simba wanapata kona lakini inaokolewa.
Dk ya 5: Mchezo umeanza kwa kasi ndogo.
Dk ya 2: Majimaji wanafika langoni mwa Simba na wanakosa nafasi ya wazi.

Mchezo umeanza.
Huu ni mtanange wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, unachezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.


NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ