JUMA MAHADHI AWAPIGIA MAGOTI YANGA,AOMBA MSAMAHA - EDUSPORTSTZ

Latest

JUMA MAHADHI AWAPIGIA MAGOTI YANGA,AOMBA MSAMAHA



Staa wa Yanga Juma Mahadhi ambaye amewahi kuonesha uwezo na kuitwa kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, hivi karibuni baadhi ya mashabiki na wapenzi wa soka waliwahi kutuhumu uwezo wa mchezaji huyo kushuka kwa uzembe ukizingatia ana umri mdogo.


Jumanne ya January 2 2018 Yanga wakielekea kuanza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya Makundi wa Kombe la Mapinduzi Juma Mahadhi kabla ya mchezo alitumia ukurasa wake wa instagram kuomba radhi uongozi na mashabiki kwa kukiri kuwa aliteleza na anaahidi kuwa Mahadhi mpya.

Juma Mahadhi baada ya kuandika ujumbe huo wa wazi kupitia ukurasa wake wa instagram jioni ya January 2 alikuwa sehemu ya kikosi cha Yanga kilichocheza dhidi ya Mlandege na kupata ushindi wa magoli 2-1 huku Juma Mahadhi akifunga magoli yote mawili na kuwapigia magoti mashabiki akiomba msamaha.

Huu ndio Ujumbe wa kuomba radhi wa Juma Mahadhi aliyouandika saa chache kabla ya kucheza game na kuifungia Yanga magoli mawili dakika ya 6 na 36.



“Asalam alykum ndg zangu katika Imani haja yangu kwenu ni kuomba radhi kwa mashabiki wangu wote na wapnz wote wa mpira wa miguu duniani, nakiri kufanya makosa hapo nyuma na nimejifunza mengi kupitia nyinyi nawaomba sana radhi”
“Haja ya moyo wangu ni kutataka kufikia malengo yangu niliyojiweka lakini kwa mwaka huu ilikua ngumu sana kutokana na changamoto nilizokutana nao”
Sasa ombi langu kwenu Mashabiki,Viongozi na bench la ufundi ni kuwamba kijana wenu nahitaj msamaha kama niliwakosea bado nahitaji nafasi naamin siwez kurudia kosa kwani nimejifunza mengi naahidi kuwa Mahadhi mpya”

“Naomba Imani yenu kwangu na kama mnaona bado naitajika katika timu yangu pendwa Yanga SC, tumaini langu kilio changu kimewafikia nahitaji sasa kuanza mwaka mpya nikiwa kijana mwema na mpya Asanteni sana nawapenda wote”EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz