JOHN BOCCO MCHEZAJI ANAYEKUMBUKWA NA KASEJA KWA HAYA - EDUSPORTSTZ

Latest

JOHN BOCCO MCHEZAJI ANAYEKUMBUKWA NA KASEJA KWA HAYA





Goli la leo la John Bocco dhidi ya Kagera Sugar limemfanya Bocco kuwa mchezaji aliyefunga magoli mengi zaidi dhidi ya golikipa Juma Kaseja.

Bocco amefikisha jumla ya magoli 10 dhidi ya Kaseja anaeitumikia Kagera Sugar kwa sasa lakini akiwa amewahi kuzichezea Simba, Yanga, Mbeya City na timu ya taifa ya Tanzania ‘Taifa Stars’.

Magoli hayo Bocco ameyafunga katika mashindano tofauti yaliyomkutanisha na Kaseja ambaye ni golikipa wa muda mrefu kwenye ligi ya Tanzania.
Ligi kuu Tanzania bara (VPL) muda wote-magoli matano
Robo fainali Kagame Cup 2012 (Azam vs Simba)-magoli matatu (hat-trick)
Ngao ya Jamii (Simba vs Azam)-goli moja
Mechi ya kirafiki (mechi ya hisani kuchangia walemavu) Azam vs Simba-goli moja.

Goli moja moja limeondolewa ambalo Bocco alimfunga Kaseja kwenye mchezo wa ligi Mbeya City vs Azam mchezo ambao Azam ilipoteza pointi zote licha ya kushinda kwa sababu ilimchezesha Erasto Nyoni ambaye alikuwa ana kadi zisizomruhusu kucheza.

“Kaseja ni golikipa mzuri namheshimu, amedaka kwa muda mrefu ameweza kujitunza kwa muda mrefu nampongeza kwa hilo. Kwa upande wangu kumfunga Kaseja ni jitahada tu”-amesema Bocco baada ya kuweka rekodi ya kuwa mshamuliaji aliyemfunga magoli mengi kati ya wachezaji waliowahi kumfunga Kaseja.

“Yeye yupo kwenye nafasi ya kufunga mimi nipo kwenye kuzuia, yeyote atakaepata nafasi nzuri anaweza kuitumia, yeye kapata nafasi kaitumia hata mimi ningepata nafasi nzuri ningeweza kuzuia. Mpira ni mchezo wa makosa, tumefanya makosa mawili wameweza kutumia nafasi”-maneno ya Kaseja ambaye ameruhusu magoli 10 tangu aanze kukutana na John Bocco.
NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO


EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz