HUYU HAPA MWANASAYANSI ALIYEDANGANYA KUONGEZEKA SM 9 AKIWA ANGANI - EDUSPORTSTZ

Latest

HUYU HAPA MWANASAYANSI ALIYEDANGANYA KUONGEZEKA SM 9 AKIWA ANGANI


Mwanasayansi Norishige Kanai (kushoto)

Mwanasayansi wa anga za juu wa Japan ameomba msamaha kwa kusema kimakosa kuwa alikuwa amekuwa kwa sentimita 9 tangu awasili kwenye kituo cha kimataifa cha anga za juu (ISS) wiki tatu zilizopita.

Norishige Kanai alisema kwa hakika alikuwa amekuwa kwa sentimita mbili akilaumu kasoro ya vipimo.

"Ninaomba msamaha kwa kuandika habari za uongo kama hizo," aliandika kwa lugha ya kijapani.

Madai yake ya awali ya uongo yalizua maoni miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii. Wanasayansi kwa kawaida hukua kwa takriban sentimita 2-5 wanapokuwa katika kituo cha anga za juu.

Bw. Kanai awalia alikuwa ameandika kwa lugha ya kijapani akisema, "Habari za asubuhi nyote, nina tangazo muhimu kwa kila mtu. Tulimpimwa miili yutu baada ya kufika angani na wao, wao, wao, nimekua kwa sentimita 9!

"Nimekua kama mmea kwa wiki tatu tu. Kitu kama hiki hakijafanyika tangu nilipokuwa shule ya upili. Nina hofu ikiwa nitatoshea kwenye chombo cha Soyuz wakati nitarudi duniani.

Chombo cha Soyuz kinachowasafirisha wanasayansi kwenda angani na kurudi kina vipimo vya urefu wa kuketi na ikiwa mtu atakuwa mrefu zaidi itakuwa ni tatizo kubwa.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati.Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz