HABARI NA TETESI ZA SOKA LA ULAYA IJUMAA YA LEO 26.1.2018 - EDUSPORTSTZ

Latest

HABARI NA TETESI ZA SOKA LA ULAYA IJUMAA YA LEO 26.1.2018



Mshambuliaji wa Paris St-Germain na Brazil Neymar ataruhusiwa kujiunga na Real Madrid, lakini kwa makubaliano ya iwapo ataisaidia timu hiyo ya Ufaransa kubeba kombe la vilabu bingwa Ulaya kulingana na rais wa timu hiyo Nasser Al-Khelaifi .Mchezaji huyo mwenuye umri wa miaka 25 ana ndoto ya kuichzea timu hiyo. (Goal)

Mazungumzo yamegonga mwamba kati ya Arsenal na Borussia Dortmund kuhusu makubaliano ya mshambuliaji wa klabu hiyo na Garbon Pierre -Emrick Aubameyang kwenda Arsenal.

Dortmund pia inatarajiwa kusitisha majadiliano ya kumsajili mshambuliaji wa Arsenal Olivier Giroud .Mchezaji huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 31 anadaiwa kutaka kushirikishwa katika kila mechi. (Mail)

Chelsea inataka kumsajili Giroud , ikiwa na matumani ya kutaka kumshawishi kuhamia magharibi mwa mji huo. (Mirror)Image captionManchester City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte wikendi hii

Manchester City inatarajia kukamilisha usajili wa beki wa Athletic Bilbao Aymeric Laporte wikendi hii. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 23 amebadilisha nia yake baada ya kukataa uhamisho wa kueleka City miezi 18 iliopita.{Mirror}

Wakati huohuo mmiliki wa Chelsea Abrahamovic amekasirishwa na mkufunzi Conte baada ya kocha huyo kujitenga na usajili wa mchezaji mpya msimu huu. (Star)
Lucas Moura, 25, alikutana na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy mjini London siku ya Alhamisi

Winga wa PSG Brazil Lucas Moura, 25, alikutana na mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy mjini London siku ya Alhamisi kuzungumzia uhamisho wa kuelekea Spurs. (RMC - in French)

Diafra Sakho ameiambia West Ham anataka kuondoka na klabu ya Ufaransa ya Rennes ndio anakoelekea . Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 28 kutoka Senegal hajashirikishwa katika mechi nyingi za West Ham msimu huu (Sun)Image captionWest Ham inalenga usajili wa nahodha wa Fulham Tom Cairney

West Ham inalenga usajili wa nahodha wa Fulham Tom Cairney na wako tayari kutoa dau la £15m kumnunua mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 27 kutoka Uskochi. (Sky Sports)

West Ham imewasilisha ombi la £12m kumsajili kiungo wa kati wa Norwich na Uingereza James Maddison, 21. (Guardian)

Ombi la pili la Crystal Palace kutaka kumsajili beki wa Lille Ibrahim Amadou limekataliwa. Palace ilikuwa imehusishwa na uhamisho wa mchezaji huyo wa Cameroon mwenye umri wa miaka 24 mapema mwaka huu. (Sky Sports)Image captionMshambuliaji wa zamani wa Fulham, Reading na Urusi Pavel Pogrebnyak

Mshambuliaji wa zamani wa Fulham, Reading na Urusi Pavel Pogrebnyak, 34, alichiliwa na Dynamo Moscow kwa sababu ya kuhudhuria mechi ya Juventus nchini Itali , licha kuambia klabu hiyo kwamba alikuwa mgonjwa sana kuichezea (Sport Express - in Russian)

Mshambuliaji wa Leicester na Uingereza Jamie Vardy anatarajiwa kukabiliana na ,mwanafunzi aliyehitimu kutoka chuo chake cha soka cha V9 Academy, Alex Penny, wakati Leicester itakapocheza dhidi ya Peterborough katika kombe la FA raundi ya nne siku ya Jumamosi. (Sky Sports)Image captionMkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa angependelea kufanyakazi katika shamba badala ya kuifunza Arsenal au Barcelona

Mkufunzi wa Tottenham Mauricio Pochettino anasema kuwa angependelea kufanyakazi katika shamba badala ya kuifunza Arsenal au Barcelona , lakini raia huyo wa Argentina ambaye ana umri wa miaka 45 hajapinga kuelekea Real Madrid.(Express)

Arsenal wanajiandaa kumsajili kiungo wa kati wa Corinthians na mchezaji wa timu ya Brazil isiozidi umri wa miaka 20 Maycon, 20. (Sun)Image captionMkufunzi wa Leicester Claude Puel anasema kuwa winga Riyad Mahrez hatahamia klabu nyengine yoyote

Mkufunzi wa Leicester Claude Puel anasema kuwa winga Riyad Mahrez hatahamia klabu nyengine yoyote wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 kutoka Algeria alipigwa picha akiwa katika uwanja wa Emirates akitazama mechi ya kombe la Carabao kati ya Arsenal na Chelsea siku ya Jumatano, lakini Puel amesisitiza kuwa anawatafutia wachezaji Leicester. (Mirror)

Sandro Ramirez ameambia Everton anataka kuondoka katika klabu hiyo. Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 22 kutoka Uhispania yuko tayari kurudi nyumbani huku klabu ya La Liga ya Sevilla ikimnyatia. (Mail)
Kiungo wa kati wa West Brom na Ireland Kaskazini Chris Brunt, 33, anakaribia kusaini kandarasi mpya katika klabu hiyo.(Birmingham Mail)
NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz