BREAKING NEWS: BAADA YA KUITESA SINGIDA, HANS POPPE AMPA GARI SAID NDEMLA - EDUSPORTSTZ

Latest

BREAKING NEWS: BAADA YA KUITESA SINGIDA, HANS POPPE AMPA GARI SAID NDEMLA


Image result for Said Hamis Ndemla.

NDG MSOMAJI WA EDUSPORTSTZ UNAKUMBUSHWA KUSUBSCRIBE NA KUFOLLOW WEB YETU PAMOJA NA MITANDAO YETU YA KIJAMII CHINI YA POSITI HII ILI KUTUMIWA UPDATES ZOTE ZA AJIRA, MICHEZO, HABARI, SCHOLARSHIPS PAMOJA NA MASTORI YA MASTAA NA VIONGOZI MBALIMBALI. EDUSPOTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI.

Mwenyekiti wa Kamtai ya Usajili ya Simba, Zacharia Hans Poppe ametoa zawadi ya gari kwa mchezaji wa Simba, Said Hamis Ndemla.


Hans Poppe ametangza kumpa Ndemla gari baada ya kuonyesha kiwango kizuri cha kuvutia katika mechi dhidi ya Singida United, leo.


Simba imeshinda kwa mabao 4-0 katika mechi hiyo ilikuwa inasubiriwa kwa hamu kubwa na mashabiki wa soka nchini. Ndemla alitengeneza mabao mawili moja akifunga Emmanuel Okwi na jingine Asante Kwasi.


Akizungumza na SALEHJEMBE hivi punde, Hans Poppe amesema mechi ya leo imekuwa ni fainali ya uamuzi wake lakini amekuwa akimfuatilia Ndemla.


“Nilikuwa nikimfuatilia kama ambavyo nimekuwa nikisema nahitaji mchezaji mwenye nidhamu na ambaye hawezi kubadilika. Utaona Ndemla amekuwa benchi lakini akiingia uwanjani anaonyesha mchango wake,” alisema.


“Tena pamoja na kukaa benchi, hakuwahi kuonyesha utovu wa nidhamu. Badala yake kila akipata nafasi amekuwa akijituma na kuisaidia timu.”


Hii ni mara ya pili Hans Poppe anatoa gari kwa mchezaji wa Simba. Alianza na Hussein Zimbwe aliyempa gari aina ya Toyota Raum. Lakini akaonyesha gari aina ya Toyota Lactic na kusema atapewa mchezaji atakayefanya vizuri.




Kuhusiana na aina, leo amesema: “Aina utaijua baadaye ila gari haiko mbali. Hivyo tutaangalia siku yenye nafasi atakabidhiwa.”
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati. BOFYA HAPA KUJIUNGA NA INNOVATION FURSA CHALLENGE http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz