NYOTA WA SIMBA JAMAL MNYATE AOMBA BARUA KUONDOKA - EDUSPORTSTZ

Latest

NYOTA WA SIMBA JAMAL MNYATE AOMBA BARUA KUONDOKA



Jamal Mnyate.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Jamal Mnyate, ameomba barua kwa uongozi wa timu hiyo itakayomruhusu kuondoka na kwenda kwenye klabu nyingine kucheza soka.

Awali, kulikuwepo na taarifa za mshambuliaji huyo kuwepo kwenye orodha ya wachezaji watakaoachwa kwenye usajili huu wa dirisha dogo lililofunguliwa Novemba 15, mwaka huu.

Mchezaji mwingine anayetajwa kuachwa ni mshambuliaji Juma Liuzio ambaye yeye uongozi wa Simba umepanga kumtoa kwa mkopo.

Kwa mujibu wa taarifa ambazo Championi Jumatatu limezipata, mshambuliaji huyo anaomba barua hiyo ya kuachwa ili aende zake akaichezee Lipuli FC inayonolewa na Selemani Matola.

Aliongeza kuwa, mshambuliaji huyo tayari amekutana na mabosi wake huku akiahidiwa kupatiwa barua hiyo ya kuondoka Simba baada ya kukosa nafasi ya kucheza.

“Mnyate hatutakuwa naye katika mzunguko wa pili wa ligi kuu, kwani yeye mwenyewe ameomba barua ya kuachwa baada ya kuwepo taarifa za kutolewa kwa mkopo.

“Hivyo, yeye mwenyewe ameomba aachwe moja kwa moja na siyo kwa mkopo kama wanavyotaka wenyewe Simba na maamuzi hayo ameyatoa baada ya kuona anakosa nafasi ya kucheza,” alisema mtoa taarifa huyo.


Alipotafutwa Kocha Mkuu wa Lipuli FC, Selemani Matola kuzungumzia hilo juu ya mshambuliaji huyo kuomba aende huko, alisema: “Ni kweli kabisa hizo taarifa, kama mambo yakienda vizuri basi Mnyate tutakuwa naye katika mzunguko wa pili wa ligi kuu.

“Kwani yeye mwenyewe ameonyesha nia ya kuja kuichezea Lipuli, hivyo ninamkaribisha na kama unavyojua timu yangu ina tatizo katika safu ya ushambuliaji, ninaamini kama akija yeye basi timu itaimarika zaidi.”


NINI MAONI YAKO? TUACHIE UJUMBE WAKO HAPA

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz