MWALICHOKISEMA VIONGOZI WA SIMBA BAADA YA KUMTEMA OMOG - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 24 December 2017

MWALICHOKISEMA VIONGOZI WA SIMBA BAADA YA KUMTEMA OMOGBaada ya Kutolewa Jana Timu ya Simba Yasikia Maoni ya Mashabiki na Wanachama Wake Je Omog Kutimuliwa?
Klabu ya Simba na kocha wake mkuu Joseph Omog, wameamua kwa pamoja kuvunja mkataba baina yao kwa makubaliano maalum yanayozingatia maslahi ya pande zote mbili.


Klabu inamshukuru kocha Omog na inamtakia kila la kheri kwenye maisha yake nje ya Simba.


Kwa wakati huu Timu yetu itakuwa chini ya kocha msaidizi Masoud Djuma na itaendelea na mazoezi kesho,na kupumzika siku ya Jumatatu kwa mapumziko ya sikukuu ya Christmas na itaingia kambini Jumanne kabla ya safari ya Mtwara,ambapo tutacheza na Timu ya Ndanda kwenye mchezo wa Ligi kuu wiki ijayo.


Pia kwa niaba ya uongozi, benchi la ufundi na wachezaji.Tutumie nafasi hii kuwaomba radhi sana Wanachama na washabiki wetu kwa matokeo ya jana, sote tumeumia ila ndio mchezo wa mpira ulivyo, na tuwaombe muwe watulivu katika kipindi hiki ili tufikie malengo yetu.


Mwisho


Klabu inawatakia nyote Sikukuu njema ya Noeli na mapumziko mema ya wikiendi.


IMETOLEWA NA....


Haji S MANARA
Mkuu wa Habari Simba ScSIMBA NGUVU MOJA
EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment