MURSHID JUUKO AMALIZANA NA SIMBA KIMYAKIMYA - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Tuesday, 12 December 2017

MURSHID JUUKO AMALIZANA NA SIMBA KIMYAKIMYA
Uongozi wa klabu ya Simba ililazimika kufanya umafia na kuyamaliza mambo kimyakimya huku watu au mashabiki wake wakiendelea kuwa na hofu.

Wakati mkataba wa beki wake Juuko Murshid ukienda ukingoni, Simba ilimuita mezani na kumsainisha mkataba wa miaka miwili fasta.

Pamoja na kufanya hivyo ukaendelea kukaa kimya bila ya kueleza jambo na hivyo kuwafanya watani wake Yanga kuendelea kumfuatilia wakitaka kuimarisha kikosi chake katika safu ya ulinzi.

Hata hivyo, Yanga imekuja kushituka mwishoni kwamba Simba ilishamaliza mchezo na kukaa kimya kabisa.

Kwa sasa, Juuko anaitumikia The Cranes katika michuano ya Chalenji inayoendelea nchini Kenya.

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno