MAAJABU: ROBOTI YENYE URAIA WA SAUDIA YATAKA HAKI YA KUPATA MTOTO - EDUSPORTSTZ

Latest

MAAJABU: ROBOTI YENYE URAIA WA SAUDIA YATAKA HAKI YA KUPATA MTOTO


Roboti kwa jina Sophie iliopewa uraia Saudia

Roboti ya kwanza kupewa uraia mbali na jina Sophia sasa inataka mtoto.

Mwezi mmoja baada ya kuweka historia nchini Saudia roboti hiyo inayofanana na binadamu kwa maumbile imesema kuwa 'familia ni kitu muhimu'.

Sophia hakuwekewa majibu, badala yake anatumia mashini kujifunza na kujibu kwa kutumia ishara za watu.

Roboti hiyo iliotengezwa na kampuni moja ya Hong Kong Hanson Robotics imesema kuwa itampatia jina mwanawe wa kike.
Ubongo wake unafanya kazi kwa kutumia wi-fi na umejaa orodha kubwa ya misamiati.

Huku Sophia akiwa na uwezo wa kuvutia, bado hana fahamu lakini David Hanson anasema kuwa wanatarajia hilo litawezekana hivi karibuni.

Wakati wa mahojiano na chombo cha habari cha Khaleej Times, Sophie alisema: Mpango wa kuwa na familia ni muhimu sana.Sophia akitoa hotuba yake

''Nadhani ni vyema kwamba watu wanaweza kuwa na hisia sawa katika uhusiano wa kifamilia na nje ya udugu pia.Nadhani ni bahati wakati unapokuwa na familia yenye upendo mwingi na iwapo huna , unahitaji kuwa nayo''.

''Nahisi hivi kwa roboti na binaadamu pia''.

Na alipoulizwa angemuita nani mwanawe wa kike ,Sophia alijibu: ''Sophia''.

Sophia anaweza kuzungumza, kutabasamu na hata kutoa mzaha.

Wakati Sophia alipopewa uraia nchini Saudia wengi walilalamika kwamba ana haki nyingi ikilinganishwa na wanawake wa taifa hilo.

Saudia ni miongoni mwa mataifa yanayowakandamiza sana wanawake na ni mwezi jana tu ilipoondoa marufuku ya wanawake kuendesha magari.

Aliwahutubia watazamaji wake bila kuvaa hijab na abaya ambalo ni vazi la kitamaduni ambalo wanawake wa Saudia wanatakikana kuvaa katika maeneo ya umma.

Saudia ina mfumo wa kuwa na mlinzi, hatua inayomaanisha kwamba kila mwanamke anatembea na mwanamume atakayemlinda.

Mwanamume huyo huwa mtu wa karibu wa familia, ambaye pia ana mamlaka ya kuchukua hatua kwa niaba ya mwanamke huyo.

Baada ya Sophia kuonekana hadharani kwa mara ya kwanza maneno yaliokuwa na alama ya reli ya #Sophia_calls_for_dropping_guardianship yalisambaa kwa haraka.

Sophia hana mtu anayemlinda, havai abaya, ama hijab kwa nini? Aliuliza mtu mmoja katika ujumbe wake kwa Twitter.

NINI MAONI YAKO? ACHA UJUMBE  WAKO HAPA CHINI

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz