KENYA YAPETA FAINALI MICHUANO YA CECAFA - EDUSPORTSTZ

Latest

KENYA YAPETA FAINALI MICHUANO YA CECAFA


Paul Put amewaongoza Kenya kwa fainali na Cecafa chini ya mwezi mmoja baada ya kupewa mikoba kuinoa timu ya taifa hilo


Wenyeji Kenya wamefuzu kwa michuano ya ubingwa wa kanda ya Afrika mashariki na kati, maarufu kama Cecafa Senior Challenge.

Kenya wamefuzu baada ya kufunga bao muda wa ziada dhidi ya Burundi katika nusu fainali iliyochezewa mjini Kisumu, Magharibi mwa Kenya Alhamisi.

Baada ya kumaliza dakika 90 bila bao, kiungo wa kati Whyvonne Isuza alifunga bao la ushindi kipindi cha kwanza muda wa kuongezwa.



Hemed: Wachezaji wa Zanzibar katika Cecafa hawana doa

Kenya, chini ya mkufunzi wao mpya Paul Put, sasa watacheza na mshindi wa nusufainali kati ya Uganda na Zanzibar kwenye fainali Jumapili.

Ushindi huo wa Kenya umeendeleza mwanzo mzuri kwa Mbelgiji Put ambaye alichukua usukani kama mkufunzi mkuu mwezi jana.

Mada zinazohusianaEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz