HII NDO MBINU ANAYOTAKA KUTUMIA PLUIJM KUWAPIKU YANGA NA SIMBA - EDUSPORTSTZ

Latest

HII NDO MBINU ANAYOTAKA KUTUMIA PLUIJM KUWAPIKU YANGA NA SIMBA





Bosi wa benchi la ufundi la Singida United, Hans van Der Pluijm amejipanga kuzipiku Simba na Yanga katika msimamo wa Ligi Kuu Bara kwa kushinda kila mechi iliyo mbele yake akianza na Njombe Mji, kesho Jumapili.




Singida ipo nafasi ya nne ikiwa na pointi 20 nyuma ya Yanga ambayo ina pointi 21, huku Simba ikiongoza kwa kuwa na pointi 23.


Pluijm amesema anaijua Njombe ni moja ya timu nzuri kwenye ligi, lakini amejipanga kuhakikisha anafanikiwa kushinda ili kujiweka katika nafasi nzuri.




“Mechi yetu na Njombe itakuwa ngumu lakini tupo tayari kupambana ili kuweza kufanikiwa kuwa katika nafasi ya kwanza ya msimamo wa ligi, tunahitaji kujituma ili tuweze kukaa kileleni.




“Tumepitwa pointi chache na Simba na Yanga hivyo nimepanga kupambana tuwe kileleni japokuwa nitawakosa Raphael Kutinyu ambaye ni majeruhi na Juma Kennedy mwenye kadi tatu za njano.



“Ligi ni ngumu na ina ushindani, Njombe ni moja kati ya timu zenye ushindani, lakini nimewaandaa vyema wachezaji wangu kuhakikisha tunashinda,” alisema PluijmEDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
UNGANA NASI KUPITIA LIKI HIZI ILI KUTUMIWA HABARI POPOTE ULIPO

EDUSPORTSTZ NI FAHARI YA WASOMAJI

WEKA EMAIL YAKO:


Delivered by EDUSPOTSTZ
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno
EDUSPORTSTZ


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz