TFF WANENA KUHUSU SAMATTA KUELEKEA MCHEZO WAKIRAFIKI NA BENIN - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 8 November 2017

TFF WANENA KUHUSU SAMATTA KUELEKEA MCHEZO WAKIRAFIKI NA BENIN


Mbwana SamattaNahodha wa Taifa Stars ya Tanzania inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, Mbwana Ally Samatta.

Shirikisho la Soka la Tanzania (TFF) limetoa tamko kuwa sasa ni rasmi, nahodha wa Taifa Stars ya Tanzania inayodhaminiwa na Bia ya Serengeti, Mbwana Ally Samatta,

atakosa mchezo kati Tanzania na Benin utakaofanyika Novemba 12, 2017 kwa sababu ya majeraha ya goti.

Taarifa kutoka kwa matatibu wa Genk ya Ubelgiji, zinasema kwamba Mbwana Samatta anatarajiwa kufanyiwa upasuaji mdogo na mpaka kupona, madaktari wamesema itamchukua wiki nane ili kurejea uwanjani.

Kocha wa Taifa Stars, Salum Shabani Mayanga amepokea taarifa hiyo na kusema haijawa bahati kwa Stars, lakini atapanga kikosi chake vema kwa wachezaji atakaokuwa huko Benin akiwamo Abdi Banda na Farid Mussa.

Wachezaji watakaosafiri ni Aishi Manula, Peter Manyika, Gadiel Michael, Boniphas Maganga, Kelvin Yondani, Nurdin Chona, Himid Mao, Hamis Abdallah, Raphael Daudi, Mohamed Issa, Jonas Mkude, Mudathir Yahya, Simon Msuva, Shiza Kichuya, Faridi Mussa, Ibrahim Ajib, Mbaraka Yusuph na Elias Maguli.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI


SHILIKISHA WENZAKO HAPA