TETESI ZA SOKA JUMATANO YA LEO TAREHE 29.11.2017 - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Wednesday, 29 November 2017

TETESI ZA SOKA JUMATANO YA LEO TAREHE 29.11.2017


David Luiz

Real Madrid wanalenga kumsajili beki wa Chelsea na Brazil David Luiz 30 ambaye hatakikani katika uwanja wa Stamford Bridge msimu huu. (Daily Mail)

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa hajaelezwa iwapo atalazimika kuwasajili wachezaji wowote katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari iwapo mabingwa hao watetezi wanatarajiwa kuwafikia viongozi wa ligi Manchester City. (Guardian)Image captionLeroy Sane

Mchezaji wa Manchester City na raia wa Ujerumani mwenye umri wa 21 Leroy Sane atapewa kandarasi mpya na Manchester City mwishoni mwa msimu huu. (Sun)

Watford wameonya kwamba mshambuliaji wao raia wa Brazil Richarlison, 20, ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa mkataba wa miaka mitano kutoka Fluminence mnamo mwezi Agosti kwa kitita cha £11m na anavutia klabu za Tottenham na Chelsea hauzwi wakati wa dirisha la uhamisho la mwezi Januari. (London Evening Standard)Image captionAlexandro Sane

Chelsea wanatarajiwa kumnunua beki wa Juventus Alex Sandro ,26, mwezi Januari baada ya kushindwa kumsajili mshambuliaji huyo wa Brazil mwaka uliopita.(Daily Express)

Liverpool na Leicester wanaangazia kumsajili beki wa West Brom na Misri Ahmed Hegazi, 26, ambaye yuko katika mkopo kutoka klabu ya Al Ahly. (ESPN)Image captionDavid Silva

Kiungo wa kati wa Manchester City David Silva, 31, anatarajiwa kuandikisha mkataba mpya ambao utamweka mchezaji huyo wa Uhispania katika uwanja wa Etihad hadi 2020. (Daily Mirror)

City haitamuuza mlinzi wa Ufaransa Eliaquim Mangala mnamo mwezi Januari , lakini mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 hajapewa thibitisho kuhusu hatma yake katika klabu hiyo. (Goal)

Liverpool na Juventus wote wanataka kumsajili winga wa klabu ya Sporting Lisbon mwenye umri wa miaka 22 raia wa Ureno Gelson Martins. (A Bola, via Talksport)Image captionArsene Wenger

Mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger anasema kuwa afisa mkuu mtendaji wa klabu hiyo Ivan Gazidis hausiki na mpango wa kuwanunua wachezaji kufuatia mabadiliko yaliofanyika katika klabu hiyo(Daily Mail)

Mchezaji anayesakwa na klabu ya Manchester City na Napoli Sime Vrsaljko anataka kuondoka Atletico Madrid. Beki hiyo huyo mwenye umri wa miaka 25 raia wa Croatia anatafuta changamoto mpya(Talksport)Image captionAntoinne Griezman

Mshambuliaji wa Atletico Antoine Griezmann angejiunga na Arsenal mwaka 2013 lakini the Gunners wakaamua kutomsajili mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 26 na wakati waliporudi kutaka kumsajili alikataa (Daily Express)

Swansea inapigiwa upatu kumsajili mshambuliaji wa Liverpool Dominic Solanke, 20. (Wales Online)

Beki wa Arsenal na Ufaransa Laurent Koscielny, 32, anataka kumaliza mchezo wake katika klabu ya Lorient, kulingana na rais wa klabu hiyo ya Ufaransa (Canal+, via Goal)

Arsenal ni miongoni mwa vilabu kadhaa vya ligi ya Uingereza wanaotaka kumsajili Novara Calcio mwenye umri wa 20 raia wa Uholanzi Alessio da Cruz. (Daily Mirror)Image captionMshambuliaji wa Liverpool Divock Origi,

Mshambuliaji wa Liverpool Divock Origi, ambaye yuko Wolfsburg kwa mkopo hajui hatma yake katika klabu ya Anfield, huku mchezaji huyo wa Ubelgiji akiendelea kuvutia katika ligi ya Ujerumani ya Bundesliga. (Liverpool Echo)

Mshambuliaji wa Newcastle Alex Gilliead mwenye urmi wa miaka 21 ambaye yuko kwa mkopo katika klabu ya Bradford, anatakiwa na klabu ya Hull, Millwall na wapinzani wao Sunderland. (Newcastle Chronicle)

EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno