TAZAMA MATOKEO MECHI ZA JUMAMOSI EPL - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 19 November 2017

TAZAMA MATOKEO MECHI ZA JUMAMOSI EPL


Mohammed Salah wa Liverpool akicheka na wavu dhidi ya Southampton


Manchester City ilionyesha mchezo mwengine mzuri katika ushindi dhidi ya Leicester ambao umeimarisha uongozi wake katika kilele cha jedwali la ligi ya Uingereza.

Kikosi cha Pep Guradiola kiliendeleza msururu wake wa matokeo mazuri baada ya likizo ya mechi za kimataifa kwa kujipatia ushindi wa 16 mfululizo katika mashindano yote kupitia uongozi wa mshambuliaji wao Gabriel Jesus kabla ya kiungo wa kati De Bryuine kufunga mkwaju mkali ambao kipa wa Leicester alishindwa kuuona.

Wakati huohuo mabingwa watetezi Chelsea walipata ushindi rahisi dhidi ya West Brom na kumuongezea presha kocha wa West Brom Tony Pulis.

Alvaro Morata alifunga bao lake la nane katika ligi baada ya kufunga mpira uliopanguliwa na kipa Ben Foster kufuatia shambulio la Eden Harzard.Kiungo wa kati wa ManCity De Bryuine akifunga bao zuri baada ya pasi nzuri ya Leroy Sane

Hazard alifunga bao la pili muda mfupi baadaye wakati alipochukua pasi ya kisigino ya Morata, akamchenga Foster na kucheka na wavu kabla ya Marcos Alonzo kufunga bao la tatu kutoka mkwaju wa adhabu wa Cesc Fabregas.

Katika kipindi cha pili Harzard alifunga bao lake la pili kutoka maguu 18 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa fabregas.

Kwengineko Mohamed Salah aliendeleza umahiri wake kwa kuipatia Liverpool mabao mawili huku timu hiyo ikiilaza Southampton kwa urahisi na kujipatia ushindi wa tatu mfululizo kwa mara ya kwanza 2017.Eden Hazard akifunga dhidi ya West Brom

Baada kuonyesha mchezo mzuri kutoka dakika za kwanza ,mshambuliaji wa Misri Salah alifunga bao zuri kutoka miguu 18 ,baada ya Dusan Tadic kufanya masihara na kupoteza mpira karibu na eneo hatari.

Mshambuliaji huyo aliipatia timu hiyo ya nyumbani bao la pili kufuatia pasi ya Phillipe Coutinho.

Hakuna mchezaji wa ligi ya Uingereza mwenye mabao mengi katika mashindano yote kama Salah msimu huu na ijapokuwa alitulia baada ya kipindi cha kwanza Coutinho alichukua uongozi na kufunga kufuatia mpira uliopanguliwa na kipa baada ya shambulizi la Roberto Firmino.

Matokeo ya EPL JumamosiMatokeo ya ligi ya Epl Jumamosi

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment