RAGE ATOA YA MOYONI; MUKUDE HASTAHILI HATA KUCHEZA SIMBA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 6 November 2017

RAGE ATOA YA MOYONI; MUKUDE HASTAHILI HATA KUCHEZA SIMBA

 MKUDE SIMBA
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Simba, Ismail Aden Rage, amesema kiungo Jonas Mkude hastahili kucheza soka kwenye ligi ya Bongo kutokana na kiwango chake.

Rage ndiye kiongozi aliyemuuza aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Mbwana Samatta kwenda Klabu ya TP Mazembe ambaye kwa sasa anaichezea Genk ya Ubelgiji.

Rage alisema kuwa, Mkude ni miongoni mwa wachezaji wazuri na hawastahili kuchezea katika klabu za hapa Bongo na badala yake anastahili kucheza katika timu za nje kama TP Mazembe na hata Ulaya, kikubwa ni kujitambua kwa mchezaji husika na kujituma ili aweze kufanikisha jambo hilo. “Mkude ni mchezaji mzuri, hakuna ubishi katika hilo na anayeamua kumchezesha ama kutomchezesha ni kocha.

“Nimpongeze kocha wa timu ya taifa, Salumu Mayanga kuweza kumrejesha tena katika kikosi cha timu ya taifa kwani ni mchezaji mwenye uwezo na walifanya makosa kumuacha katika kikosi hicho kwa kuwa ana uwezo. Nampenda kwa kweli.

“Ni mchezaji mwenye ‘future’ nzuri, lazima tukubaliane ana uwezo wa kucheza hata katika timu za nje kama TP Mazembe, Casablanca hata Ulaya, ninamtabiria atakuwa mchezaji mkubwa hapo baadaye,” alisema Rage.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment