PARDEW KUWA MENEJA MPYA WA WEST BROM - EDUSPORTSTZ

Latest

PARDEW KUWA MENEJA MPYA WA WEST BROM


Uteuzi wa Alan Pardew (kulia) una maana kwamba sasa yeye na Tony Pulis wamekuwa wakufunzi wa West Brom na Crystal Palace Ligi ya Premia

West Brom wamemteua meneja wa zamani wa Newcastle na Crystal Palace Alan Pardew kuwa meneja wao mpya.

West Brom walimfuta kazi Tony Pulis mnamo 20 Novemba baada yao kucheza mechi 10 Ligi ya Premia bila kushinda mechi hata moja.

Walikuwa alama moja pekee juu ya eneo la kushushwa daraja.

Pardew, 56, amekuwa bila kazi tangu alipofutwa na Crystal Palace Desemba 2016.

Ametia saini mkataba wa kudumu hadi msimu wa 2019-20, na sasa amekuwa meneja wa sita kuteuliwa Albion tangu 2011.

"Nimefurahishwa sana na fursa hii ambayo nimepewa na Albion na nasubiri kwa hamu kuanza kazi na kikosi ambacho ninaamini kina wachezaji wenye vipaji sana," Pardew amesema.

"Kibarua cha kwanza kitakuwa kupata matokeo yatakayotuinua kwenye jedwali."

Mechi yake ya kwanza usukani itakuwa dhidi ya Palace ligini uwanjani Hawthorns Jumamosi, 2 Desemba (15:00 GMT).

Albion kisha watasafiri Liverpool na Swansea kabla ya kucheza nyumbani dhidi ya Manchester United.

Pardew, ambaye amewahi kuwa mkufunzi Reading, West Ham, Charlton na Southampton katika kipindi cha miaka 18 alishindwa fainali Kombe la FA mara mbili akiwa meneja.

Alitawazwa meneja bora wa mwaka na mameneja 2012 baada ya Newcastle kumaliza nafasi ya tano ligini.

Pardew Ligi ya Premia

Pardew alishinda 34.3% ya mechi Ligi ya Premia akiwa Palace, ukilinganisha na 37.4% akiwa Newcastle, 36.4% akiwa West Ham na 26.3% Charlton

Ushindi wake kwa jumla Ligi ya Premia ni 35.8%

Akiwa na Palace, Pardew aliibuka meneja wa kwanza Ligi ya Premia kuongoza klabu kumaliza nusu ya juu kwenye jedwali baada ya kuwa sehemu ya kushushwa daraja Krismasi.

Pardew amesimamia mechi 302.

Utata wa Pardew

Akiwa na West Ham mwaka 2006, Pardew alizozana na meneja wa Arsenal Arsene Wenger.

Januari 2014, alimtusi meneja wa Manchester City Manuel Pellegrini akiwa meneja Newcastle.



EDUSPORTSTZ inakutakia maandalizi mema ya siku. inakuomba kulike facebook page yetu au kufollow kupitia blog eneo la follow by email ili kutumiwa habari kwa wakati http://www.edusportstz.com ni fahari ya wasomaji
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz