NDEMLA KUANZA MAJARIBIO JUMATATU - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 11 November 2017

NDEMLA KUANZA MAJARIBIO JUMATATU
Kiungo Said Hamis Ndemla anatarajia kuanza majaribio katika klabu ya AFC, keshokutwa Jumatatu.


Ndemla tayari yuko jijini Stockholm jijini Sweden akijiandaa na kuanza majaribio na timu hiyo imetoa siku 14.


“Bado mechi mbili za ligi, AFC imekuwa ikipambana kubaki Ligi Kuu Sweden. Lakini Ndemla ameishapata nafasi ya majaribio na ataungana na wenzake Jumatatu,” kilieleza chanzo kutoka Sweden.


Ndemla ameondoka nchini juzi baada ya kuitumikia Simba katika mechi dhidi ya Mbeya City mjini Mbeya.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment