LIVE KUTOKA UWANJA WA SOKOINE:MBEYA CITY 0-1SIMBA (KIPINDI CHA PILI) - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 5 November 2017

LIVE KUTOKA UWANJA WA SOKOINE:MBEYA CITY 0-1SIMBA (KIPINDI CHA PILI)
Dk 49 Ambokile anajaribu kwa mara nyingine, anaachia shuti lakini goal kick

DK 47, Ambukile anaingia vizuri mbele ya Juuko lakini Zimbwe Jr anaokoa vizuri
KADI Dk 46 Ngassa analambwa kadi ya njano kwa kumuangusha Niyonzima
Dk 45 Kipindi cha pili kimeanza, taratibu mpira unafika katika lango la Mbeya City na Niyonzima anawekwa chini

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 45, Mbeya City wanaonekana kuendelea kikokaaa kutaka ksuawazisha
Dk 43 Muzamiru anachonga faulo safi, Nyoni na kipa, lakini kipa anaokoa vizuri kabisa
Dk 42 Niyonzima anawekwa chini, nje kidogo ya eneo la 18
Dk 40 sasa, bado inaonekana hakuna mashambulizi makali san ndani ya kila eneo la 18
Dk 35 Mbeya City wanarudisha mpira kwa kipa, ni hatari hapa lakini kipa anawahi na kuokoa
Dk 34 Ngassa anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, Manula anadaka unamtoka lakini anauwahi
Dk 32, mabeki City wanalazimika kufanya kazi ya ziada kumthibiti Kichuya

Dk 29 Kichuya anatoa pasi nzuri sana lakini Okwi anachelewa na mwamuzi anasema ni offside
Dk 25, Bocco anaingia vizuri kabisa lakini Kyaruzi anaokoa vizuri kabisa
Dk 22 mpira zaidi unachezwa katikati ya uwanja
Dk 17, Juuko analazimika kuokoa mpira wa kurushwa wa Mwasapili na kama angechelewa basi inekuwa shida
Dk 14 sasa, Mbeya City wanaonekana kuamka na kushambulia mfululizo wakiongozwa na Mrisho Ngassa lakini mipira yao mingi langoni mwa Simba imekuwa haina macho
Dk 10, Simba wanaingia vizuri tena, Bocco katika nafasi nzuri lakini anapoteza timing. Simba nao wanalalamika kuwa Bocco aliangushwa ndani ya 18


Dk 8, Mbeya City wanajibu mashambulizi hapa ndani ya eneo la hatari lango la Simba lakini Juuko anaosha hapa. Wachezaji City wanalalamika kuna mchezaji wa Simba ameshika pale
GOOOOOOOOOOOOOOO Dk 7 Kichuya anaipatia bao baada ya mpira mrefu kutoka katika ya uwanja kwa Mkude, mabeki wa Mbeya City kama wakazembe hivi
Dk 5, SImba wanaingia tena katika lango la City lakini umakini wakati wa kutupia krosi langoni unakuwa si mzuri
Dk 3, Simba wanafanya shambulizi kali, kipa Mbeya City analazimika kutoka nje kuokoa, lango halina mtu lakini Kichuya anabutua juuuu
Dk 1 mpira unaanza kwa kasi na krosi nzuri ndani ya lango la Simba, anaikosa hapa Babu Ally
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment