KIUNGO WA ARDERNAL CARZOLA ASEMA NUSRA AKATWE MGUU WAKE - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Sunday, 5 November 2017

KIUNGO WA ARDERNAL CARZOLA ASEMA NUSRA AKATWE MGUU WAKE
KIUNGO wa Arsenal, Santi Cazorla, amesema ilibaki kidogo akatwe mguu wake baada ya kupata jeraha mguuni ambalo limemweka nje ya uwanja kwa muda mrefu sasa.

Cazorla amesema matatizo ya msuli mkubwa wa mguu, ndiyo yaliyosababisha madhara katika mguu wake kiasi cha kutakiwa kukatwa lakini daktari alipambana kutibu tatizo lake.

Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32, hakuichezea Arsenal tangu Oktoba, mwaka jana, huku tatizo lake likionekana kuwa sugu kwa miezi 11 japokuwa sasa nafuu imeanza kuonekana.

Cazorla alikumbana na tatizo hilo la kuumia msuli mkubwa wa mguu mara mbili, lakini mara hii ya pili ndiyo iliyoonekana kuwa na tatizo zaidi kwake kiasi cha kutishia kukatwa mguu wake kutokana na maambukizi.

Cazorla alisema: “Daktari aliniambia, kama sasa naweza kutembea na mtoto wangu katika bustani iliyo nyumbani kwangu, ni jambo la kushukuru sana.

“Maambukizi yalisambaa kidogo kiasi cha kutishia kukatwa kwa mguu wangu, lakini madaktari walipambana na tatizo mpaka sasa naendelea vizuri, hakikuwa kipindi kizuri kwangu.”

Ni kiasi cha kusubiri kutazama hali ya afya ya Cazorla, japokuwa mwenyewe amesema anatarajia kurejea uwanjani akiwa fiti Januari, mwakani.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakikaEdusportstz


TANGAZA BIASHARA YAKO HAPAFor Booking>>>EMAIL: edusportstz@gmail.com
CALL>>>Voda: +255757441463JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
INSTAGRAM
FACEBOOKSUBSCRIBE YOUTUBE CHANEL
DOWNLOAD EDUSPORTS ANDROID APPLICATION CLICK HERE


Follow @bakalemwatz