JUVENTUS WALA KICHAPO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Monday, 20 November 2017

JUVENTUS WALA KICHAPO


Gianluigi Buffon (kati) amecheza mechi 627 Serie A , 20 nyuma ya rekodi ya Paolo Maldini

Gianluigi Buffon aliachwa kwenye benchi Juventus walipokuwa wanacheza dhidi ya Sampdoria, hatua ambayo huenda iliwagharimu Jumapili.

Walipokezwa kichapo cha 3-2.

Buffon aliwekwa kwenye benchi pamoja na beki Andrea Barzagli, kwa sababu wanahitaji "muda kusahau" masaibu ya kukosa kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Massimiliano Allegri aliwapumzisha wawili hao, ambao tayari wamestaafu soka ya kimataifa, baada ya Italia kushindwa na Sweden mechi za muondoano wa kufuzu.

Sampdoria waliongoza kupitia bao la kichwa la Duvan Zapata, Lucas Torreira na Gianmarco Ferrari nao wakaongeza na kufanya mambo 3-0.

Gonzalo Higuain na nguvu mpya Paulo Dybala walikomboa mawili dakika za mwisho.

Juventus wamesalia alama nne nyuma ya viongozi wa ligi Napoli ambao bado hawajashindwa.

Inter Milan waliwapiku na kuingia nafasi ya pili baada ya kuwashinda Atalanta 2-0 baadaye Jumapili.

Goalkeeper Buffon, 39 - ambaye anahitaji mechi 21 kuweka rekodi mpya ya uchezaji mechi nyingi zaidi Serie A, anapanga kustaafu mwisho wa msimu Juve wasiposhinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment