HAT-TRICK YA KURZAWA WA PSG YAZUA GUMZO KWA WADAU - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

DOWNLOAD AJIRA DAILY HAPA

Wednesday, 1 November 2017

HAT-TRICK YA KURZAWA WA PSG YAZUA GUMZO KWA WADAUMfaransa huyo amekuwa beki wa kwanza katika michuano ya nyakati hizi kufunga magoli matatu kwenye mechi moja klabu hiyo ikiiua Anderlecht


Layvin Kurzawa alikuwa na usiku mzuri dhidi ya Anderlecht kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa na ameweka historia pia.

Beki huyo alifunga magoli matatu kipindi cha pili Paris Saint-Germain walipoibuka na ushindi wa 5-0 dhidi ya mabingwa wa Ubelgiji, na kujihakikishia nafasi katika hatua ya mtoano.

Jitihada hizo zilikuwa za kwanza kwa Kurzawa kwenye timu ya PSG katika michuano ya Ulaya kadhalika mabao matatu ya mwanzo kwa klabu.


Hat-trick ni tamu, lakini Kurzawa amekuwa beki wa kwanza katika Ligi ya Mabingwa ya zama za kisasa kufikia hatua hiyo katika michuano.

OptaJean
✔@OptaJean


3 - @layvinkurzawa is the first defender to score a hat-trick in the history of the Champions League. Shh.
12:29 AM - Nov 1, 2017
1313 Replies
240240 Retweets
243243 likes
Twitter Ads info and privacyNi mchezaji wa pili wa PSG kufunga hat-trick kwenye michano ya Ligi ya Mabingwa, Zlatan Ibrahimovic akiwa wa kwanza kufanya hivyo Oktoba 2013.

Wahanga wa usiku huo walikuwa pia Anderlecht, ambao huenda wasitamani tena kukutana na PSG katika michuano ya Ulaya siku zijazo.

PSG wamefunga magoli 17 bila kuruhusu goli katika hatua ya makundi michuano ya mwaka huu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI