CHALLENGE CUP 2017 ITULETEE TASWIRA MPYA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 11 November 2017

CHALLENGE CUP 2017 ITULETEE TASWIRA MPYA

Mashindano ya kombe la Chalenji yanatarajiwa kuendelea mwaka huu kuanzia November 25 hadi
December 9, 2017 ambapo Tanzania imethibisha kushiriki mashindano hayo ambayo yalisimama kuchezwa kwa miaka miwili iliyopita.

Mashindano ya Chalenji yamepoteza mvuto na msisimko kama ilivyokuwa miaka ya nyuma, kutofanyika kwa mashindano hayo katika kipindi cha miaka miwili iliyopita mfululizo inaelezwa ni kutokana na chama mlezi (CECAFA) kutokuwa na pesa za kuendesha mashindanon hayo.

Michuano ya Chalenji kwa miaka ya hivi karibuni haijaonekana kupiga hatua kwenda mbele, kila kukicha iko palepale au wakati mwingine inaonekana kurudi nyuma. Michuano yote ya vilabu hata ile ya mataifa huwezi kutofautisha kwa ubora kutoka msimu mmoja hadi mwingine.

Wanaweka maslahi mbele kuliko mpira wenyewe na hilo linathibitika pale ambapo mashindano yalikuwa yanalazimishwa yafanyike Tanzania kwa kigezo kwamba mashabiki wanakwenda uwanjani kuangalia mechi huku Simba na Yanga zikiwekwa kwenye mashindano hata kama timu moja wapo haina sifa za kushiriki mashindano.

Inapotokea timu hizi zikashiriki (Simba na Yanga) hutengenezwa mazingira ya kuzikutanisha kwenye hatua ya nusu fainali au fainali kwa sababu wanaamini watapata pesa za viingilio kwa ajili ya kufidia gharama za uendeshaji. Kwa stahili hiyo mashindano yanapoteza mvuto na thamani .

Inabidi CECAFA watafute mbinu mbadala za kuywezesha mashindano kufanyika kwa kutafuta wawekezaji, watafute mfumo mzuri pamoja na motivation kwa mfano msimu huu mashindano yatafanyikia Kenya, basi kuwe na utaratibu mzuri wa kuwasafirisha wachezaji na wapokelewe kwa muda, wafikie kwenye hotel nzuri, washindane kweli na timu inayostahili kupata matokeo ipate.

Ikienda hivyo ushindani utarudi kama ilivyokuwa miaka ya nyuma enzi zile tunasikiliza kwenye radio kina Dominic Chilambo wanatutangazia, ushindani ulikuwepo wakati huo Zamoyoni, Majid Musisi, Jack Chamangwana wakiwa wanatesa kwenye soka la ukanda huu, mashindano yalikuwa yanamvuto.

Kina Musonye na wenzake wakikaa wakatengeneza mazingira ya timu kushindana kweli na kuweka pembeni siasa zilizozoeleka naamini kila kitu kitakuwa sawa kwa sababu lengo la mashindano haya ni zuri na ni miaongoni mwa mashindano ya muda mrefu lakini yamedumaa ukilinganisha na mashindano ya kanda nyingine za Afrika ambayo yamekuja baadae.


Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno

No comments:

Post a Comment