BUFFON AOMBA MSAMAHA NA KUSTAAFU KIMATAIFA - EDUSPORTSTZ

Latest

BUFFON AOMBA MSAMAHA NA KUSTAAFU KIMATAIFA


Kipa wa muda mrefu wa Itali Gianluigi Buffon akibubujikwa na mchozi baada ya kushindwa na Sweden

Mlinda lango wa Italia Gianluigi Buffon amesema ''anaomba radhi kwa kila mmoja kwenye soka ya Italia'' kwa kuiaga soka ya kimataifa baada ya kushindwa na Sweden katika mechi ya muondoano ya kufuzu kwa Kombe la Dunia.

Kulikuwa na wakati wa hati hati katika mechi hiyo pale De Rossi alipotakiwa kujiandaa kuingia uwanjani lakini badala yake akamuita mshambuliaji wa Napoli Lorenzo Insigne, mchezaji Ventura ilikataa kumuita licha ya shinikizo kutoka kwa vyombo vya habari vya Italia na mashabiki.

''nilisema tulikaribia kufika ukingoni na tulitakiwa kushinda ,kwa hivyo mwambie mshambuliaji huyo aanze kujiandaa! Nilimchagua Insigne pia.

''Nilidhani ni vyema kumuingiza Insigne uwanjani badala yake''

Hata hivyo, De Rossi, 34, pia hakuweza na hivyobasi Italy ilishindwa kupata goli ambalo lingewezesha mechi hiyo kwenda hadi muda wa lala salama.

Italia ilikabwa na kupata sufuri 0-0 na kukosa kufuzu kwa kombe la dunia kwa mara ya kwanza tangu mwaka 1958.

Buffon mwenye umri wa 39 , alisema : ni aibu mchezo wangu wa mwisho uliandamana na kushindwa kwetu kufuzu kwa kwa kombe la Dunia.

'' Lawana ni kwa kila mmoja watu . Hakuna anayeepuka.''

Mchezaji mwenza wa Buffon katika timu timu ya Juventus Andrea Barzagli na kiungo wa kati wa Roma Daniele de Rossi pia wamekamilisha taaluma yao ya kuichezea Italia, huku beki wa Juve Giorgio Chiellini akitarajiwa kujiunga nao. Wanne hao wameichezea Italy mara 461 kati yao.

Buffon amechezea Italy mara 175 kwa miaka taaluma ya 20 , akiongoza Itali kushinda kombe la dunia la 2006 na anaamini siku zijazo bado ziko na ufanisi mkubwa .

'' Kuna uhakika kwamba kutakuwa na manufaa katika soka ya Italia kwani tuna sifa ,uwezo na bidii na baada ya wakati mgumu huwa tunatafuta njia ya kurudi katika hali yetu , alisema.
Follow web yetu na like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika,ni rahisi mno


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz