AJIBU:TULIZENI MZUKA LIGI BADO MBICHII - EDUSPORTSTZ

Latest

AJIBU:TULIZENI MZUKA LIGI BADO MBICHII



Ajibu Awatuliza Mashabiki

STRAIKA wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema kuwa, matokeo yasiyoridhisha wanayoyapata hivi sasa, ni sehemu ya mchezo, hivyo mashabiki waendelee kuwaunga mkono.

Ajibu ametoa kauli hiyo baada ya juzi Yanga kutoka suluhu na Singida United katika mchezo wa Ligi Kuu Bara uliopigwa kwenye Uwanja wa Namfua mkoani Singida.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Ajibu alisema matokeo hayo si mazuri, lakini wanaendelea kupambana kuhakikisha wanairudisha furaha ya mashabiki kwa kufanya vizuri kwenye michezo ijayo.

“Mashabiki watulie na waendelee kutuunga mkono ili tuweze kufanya vizuri kwenye mechi zijazo kwa sababu haya matokeo hata sisi hatuyafurahii.

“Matokeo yetu dhidi ya Singida ni sehemu ya mchezo, tulijitahidi sana kuhakikisha tunapata ushindi lakini haikuwa hivyo kwa sababu na wenzetu nao walijipanga, kikubwa ifahamike wazi kwamba, ligi bado mbichi,” alisema Ajibu.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz