WANASOKA 5 WAGHARAMA KUBWA ZAIDI EPL - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 29 October 2017

WANASOKA 5 WAGHARAMA KUBWA ZAIDI EPL
1.Harry Kane. Thamani ya Kane inatajwa kukaribia thamani ya Neymar kwa sasa na Tot wanataka zaidi ya £170m kama unamtaka Kane, tayari Florentino Perez amekanusha kumhitaji Kane lakini ni wazi kwa umri wa Benzema na Cr7 lazima Perez atahitaji mtu hatari kuziba mapengo yao na ni Kane.
2.Phelippe Coutinho. Unafahamu kwamba Liverpool walikataa kiasi cha £118m kutoka kwa Barcelona? Ina maana Liverpool walitaka pesa kubwa zaidi ambapo Barca wanasema Liver walihitaji £200m na hii inamaanisha kwa sasa ni lazima uwe na kuanzia £118m ukimhitaji.
3.Kevin De Bruyne (KDB). Wakati Chelsea wakimuuza alionekana dogo wa kawaida tu lakini tangu City wamchukue kutoka Wolfburg anaonekana kati ya viungo bora kwa sasa duniani, kwa uwezo wake na thamani ya Man City baasi bila shaka ukiwa na kuanzia £110m City wanaweza kufikiria kukupa.
4.Dele Alli. Real Madrid wanamtala Ai na Kane kwa pamoja na sio rahisi hata kidogo kwani zaidi ya £240m zinaweza zikawatoka kuwanasa wote wawili, umri mdogo wa Ali, kiwango kikubwa akiwa ameweka kambani mabao 31 toka aanze Epl itakupasa uwe na £100m kumpata.
5.Eden Hazard. Jana tu ametoka kuwaumiza Fc Bournamouth bao pekee na kiwango chake kinaonekana kuzidi kuimarika baada ya majeraha msimu uliopita, Real wanamtaka na Hazard na Chelsea wako tayari kufikiria ada ya £100m.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads


For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment