SIMBA NA YANGA ZASHINDWA KUKATA KIU YA MASHABIKI - EDUSPORTSTZ

Latest

SIMBA NA YANGA ZASHINDWA KUKATA KIU YA MASHABIKI




Tambo na majivuno ya za mashabiki wa Yanga na Simba zimefikia tamati leo baada ya timu hizo kumaliza dakika 90, zikitoka sare ya kufungana 1-1

Yanga wamelazimishwa sare ya kufunga bao 1-1, na mahasimu wao Simba, katika mfululizo wa mechi za Ligi Kuu ya Tanzania Bara, huo ukiwa ni mzunguko wa nane kwa timu hizo ambazo kabla ya mchezo huo zilikuwa zinashika nafasi ya kwanza na ya pili kwenye msimamo.

Emmanuel Martin atabaki kwenye midomo ya mashabiki wengi wa Yanga, kufuatia kupoteza nafasi ya wazi dakika ya 72, akiwa amebaki yeye na kipa wa Simba Aishi Manula, ambaye alifanya kazi ya ziada baada ya kuupangua mpira huo na kuwa kona ambayo haikuzaa matunda.

Pambano hilo ambalo limehudhuriwa, na mashabiki wachache, kuliko mapambano yote ya watani wa jadi Simba na Yanga, kipindi cha kwanza timu zote ziligawana mchezo na kufanya hadi mapumziko milango kuwa migumu.


Simba ambayo iliwaazisha Emmanuel Okwi na Laudit Mavugo, walifika maranne kwenye lango la Yanga lakini mipira yao haikuwa na madhara na kipa wa Yanga Youth Rostand, alikuwa na kazi nyepesi ya kudaka mipira ambayo ilikuwa laini huku mabeki wake Kelvin Yondani na Andrew Vicent wakifanya kazi nzuri ya kumdhibiti Okwi na Mavugo, walioonekana hatari kwao.

Kiungo Papy Kabamba Tshishimbi, angeweza kuifungia Yanga bao dakika ya 27, baada ya kupiga shuti kali akiwa nje ya eneo la hatari lakini Aishi Manula alifanya kazi nzuri kwa kuupangua na kuwa kona.

Dakika ya 12, winga Geofrey Mwashiuya, alipata nafasi nzuri lakini akashindwa kuitumia vizuri baada ya shuti lake kudakwa vyema na Manula na baada ya hapo timu hizo ziliendeleza mapambano na mchezo huo kuchezwa sana kwenye eneo la katikati.

Kipindi cha pili kilianza kwa kasi na kila upande kuonekana kujipanga lakini Shiza Kichuya alifanikiwa kuifungia timu yake bao la kuongoza dakika ya 57, akimalizia mpira uliokuwa umepigwa na Emmanuel Okwi.

Bao hilo lilidumu kwa dakika mbili kwani Obrey Chirwa aliisawazishi Yanga, kwa bao safi akiungisha pasi ya Mwashiuya, ambaye katika mchezo wa leo alionekana kutokuwa makini kama inavyokuwa mechi zilizopita.

Bao hilo la kusawazisha lilionekana kuwachanganya Simba, na kujikuta wakiendelea kuwapa Yanga nafasi ya kulishambulia lango lao lakini kutokuwa makini kwa washambuliaji wake walishindwa kuzitumia vyema ili kuibuka na pointi tatu.

Simba walimtoa Mavugo na nafasi yake kuchukuliwa na John Bocco, ambaye alionekana kuongeza nguvu katika nafasi ya ushambuliaji wakati Yanga walifanya mabadili mawili kwa mpigo ambapo waliwatoa Mwashiuya na Rafael Daud na nafasi zao kuchukuliwa na Martin na Patto Ngonyani ambao nao hawakuweza kubadilisha matokeo.

Matokeo ya leo yameufanya msimamo kuendelea kubaki vilevile kwa Simba kubaki kileleni mwa msimamo wakifikisha pointi 16, sawa na Yanga lakini Simba wakiwa na idadi kubwa ya mabao ya kufunga.

Iike facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz