SHIZA KICHUYA AWEKWA SOKONI RASMI - EDUSPORTSTZ

Latest

SHIZA KICHUYA AWEKWA SOKONI RASMI

Mchezaji wa wiki Ligi Kuu: Shiza Kichuya


Uongozi wa Klabu ya Simba umemuweka sokoni kiungo mshambuliaji wake, Shiza Kichuya kwa kukaribisha ofa kutoka klabu yoyote.


Hivi karibuni Klabu ya Ismailia ya Misri ilishindwana na Simba juu ya dau la kumuuza kiungo huyo ambalo lilikuwa dogo, hivyo kusababisha uongozi wa klabu hiyo kukataa.


Kichuya ni miongoni mwa wachezaji wa Simba ambao wanacheza kwa kiwango kizuri na kuisaidia timu yake hiyo, jambo ambalo timu nyingi zimekuwa zikimnyemelea.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara, amefunguka kuwa, dili lao na Ismailia juu ya kumchukua Kichuya limekufa rasmi, lakini wamemuweka sokoni mchezaji huyo kwa timu yoyote itakayomhitaji.


“Ile dili kati yetu na Ismailia ilishakufa rasmi kwa sasa hakuna ishu ya Kichuya kwenda huko, lakini tupo tayari kupokea ofa yoyote ile, iwapo kuna timu itamhitaji tutakuwa tayari kumuuza mchezaji huyo.


“Simba tumekuwa na desturi ya kuwaachia wachezaji wetu kuwauza pale tunapofanikiwa kupata timu ya kucheza, hivyo mchezaji yeyote yule atakayetakiwa tutakuwa tayari kumuachia,” alisema Manara.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz