RAIS TFF KUCHAGULIWA KAMATI YA CHAN - EDUSPORTSTZ

EDUSPORTSTZ

BREAKING

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 27 October 2017

RAIS TFF KUCHAGULIWA KAMATI YA CHANShirikisho la Mpira wa Miguu Africa (CAF), limemtua Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia kuwa Mjumbe wa Kamati ya Maandalizi ya Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika – CHAN.


Rais Karia ameteuliwa kuwa miongoni mwa wajumbe 26 wanaounda kamati hiyo yenye jukumu la kuhakikisha maandalizi ya mashindano hayo yanakwenda vizuri.

Wakati huohuo, Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya CAF, Leodegar Tenga ameteuliwa kushika nafasi ya Makamu wa Rais kwenye kamati ya maendeleo ya soka la ufukweni na Futsal.

Sambamba na uteuzi huo, Tenga pia ameteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Kamati ya Maendeleo na Ufundi ya CAF yenye wajumbe 17.

Naye Lina Kessy kutoka Tanzania ameteuliwa katika kamati ya watu 15 ya maandalizi ya soka la wanawake wakati Mtanzania mwingine Paul Gaspar Marealle akiteuliwa kwenye kamati ya tiba.

Akizungumzia uteuzi huo, Rais Karia amesema amepokea vizuri uteuzi huo na atashirikiana na wenzake 25 kufikia malengo yaliyowekwa kwa ajili ya kamati hiyo.

“Uteuzi huu utanipa uzoefu kuelekea kwenye uenyeji tuliopewa kwenye mashindano ya vijana ambayo Tanzania tutaandaa fainali za Africa za vijana AFCON mwaka 2019,” amesema.

Akizungumzia kuhusiana na jukumu hilo zito la Kamati, Rais Karia amesema: “Nimeingia kuongoza mpira, uwezo ninao na kama CAF wameona uwezo wangu, nitafanya jukumu hilo kwa uwezo wangu wote.”

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI