OMOG:KWASASA TUNAWAZA NAMNA YA KUISHINDA NJOMBE MJI HATUIWAWAZI YANGA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 20 October 2017

OMOG:KWASASA TUNAWAZA NAMNA YA KUISHINDA NJOMBE MJI HATUIWAWAZI YANGA

Kikosi cha Simba, wiki ijayo kinatarajiwa kwenda visiwani Zanzibar kwa ajili ya kujiandaa na
mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya watani zao wa jadi, Yanga utakaopigwa Oktoba 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar.
Simba itaondoka jijini Dar kwenda Zanzibar baada ya mchezo wao wa kesho Jumamosi dhidi ya Njombe Mji utakaopigwa kwenye Uwanja wa Uhuru.


Mmoja wa wachezaji wa kimataifa wa Simba ambaye hakupenda kuandikwa jina lake, ameliambia gazeti hili kuwa tayari wamepewa taarifa za kwenda Zanzibar kuweka kambi kwa ajili ya kuiwinda Yanga.


“Tumeambiwa mchezo wetu wa Jumamosi dhidi ya Njombe Mji ukimalizika, basi tujiandae na safari ya kwenda Zanzibar kuweka kambi ya muda mfupi kujiandaa na mechi ijayo dhidi ya Yanga.


“Nadhani uongozi unajua kule Zanzibar ni sehemu tulivu ndiyo maana imekuwa ikipenda kutupeleka kwenda kuweka kambi kama ilivyokuwa hivi karibuni tulipokuwa tukijiandaa na mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Yanga,” alisema mchezaji huyo.Alipoulizwa Kocha Mkuu wa Simba, Joseph Omog raia wa Cameroon kuhusu mipango aliyoiweka kabla ya kuikabili Yanga, alisema: “Ngoja kwanza tumalizane na Njombe ndiyo nitaanza mikakati ya kuikabili Yanga. Siwezi kuidharau Njombe ambayo ndiyo tunapambana nayo kabla ya Yanga, hivyo akili yetu kwa sasa ipo kwa Njombe na si Yanga
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment