NYEPESI NYEPESI ZA SOKA - EDUSPORTSTZ

Latest

NYEPESI NYEPESI ZA SOKA




Messi afunga bao la 100, huku Barcelona ikiilaza Olympiakos


Messi afunga bao la 100, huku Barcelona ikiilaza Olympiakos

Lionel Messi alifunga bao lake la 100 barani Ulaya huku Barcelona ikifanya mechi hiyo kuwa rahisi licha ya kadi nyekundu aliyopewa Gerard Pique na kuilaza Olympiakos katika kombe la vilabu bingwa.

Raia huyo wa Argentina mwenye umri wa miaka 30 alifunga mkwaju wa adhabu na kuwanyamazisha wenyeji wao baada ya mchezaji wa timu hiyo Dimitris Nikolaou kujifunga mapema.

Messi baadaye alimpatia pasi Lucas Digne aliyefunga bao la tatu kabla ya kichwa kizuri cha Nikolaou kupata bao la kufutia machozi.

Pique alipewa kadi ya pili ya njano baada ya kuunawa mpira.

Beki huyo wa kati alitumia mkono wake kuuweka mpira katika eneo hatari baada ya shambulio la Gerard Deulofeu kupanguliwa na kumrudia yeye
.
Conte amtaka Mourinho kuwacha kuzungumzia Chelsea
Conte amtaka Mourinho kuwacha kuzungumzia Chelsea

Mkufunzi wa Chelsea Antonio Conte anasema kuwa mkufunzi mwenza katika klabu ya Manchester United Jose Mourinho anafaa kujitazama badala ya kuijadili Chelsea

Conte ameonyesha wasiwasi mkubwa kuhusu kikosi chake cha Chelsea kufuatia misururu ya majeraha msimu huu na kusema kuwa sare ya 3-3 dhidi ya Roma katika michuano ya vilabu bingwa imekifanya kikosi chake kuwa katika hali ya dharura.

Mourinho ambaye amewahi kuifunza Chelsea mara mbili alinukuliwa akisema kuwa kuna wakufunzi wengine ambao hupenda kulalama sana kuhusu majeraha.

''Kila wakati Mourinho lazima azungumzie kile kinachoendelea Chelsea," alisema Conte

Alipoulizwa kuhusu matamshi ya Mourinho ambayo hayakumlenga Conte moja kwa moja , kocha huyo wa Itali aliongezea: Kila mara , pia msimu uliopita, nadhani ni wakati anafaa kuzungumzia kuhusu kikosi chake na ajitazame badala ya kutazama wenzake.

Eden Hazard ainusuru Chelsea katika sare ya 3-3 dhidi ya Roma
Eden Hazard akifunga mojawapo ya mabao yake mawaili dhidi ya AS Roma

Eden Hazard aliwaokoa Chelsea's kuendeleza msururu wao wa kutofungwa katika kombe la vilabu bingwa baada ya Roma waliotawala mechi hiyo kutoka nyuma na kuongoza katika kiputi kilichojaa mbwembwe za kila aina katika uwanja wa Stamford Bridge.

Hazard alifunga bao kila kipindi cha mchezo ,mwanzo akifunga kichwa kilichosawazisha matokeo kufuatia krosi ya Pedro zikiwa zimesalia dakika 15 mechi kukamilika katika kundi C.

Mshambuliaji huyo wa Ubelgiji alikuwa ameipatia Chelsea uongozi wa mabao mawili katika kipindi cha kwanza baada ya David Luiz kuiweka Chelsea kifua mbele.

Lakini timu hiyo ya ligi ya Serie A iling'ang'ana huku Aleksandar Kolarov akifunga kabla ya Edin Dzeko kufunga mabao mawili katika dakika sita.

Shambulizi lake la kwanza ulikuwa mpira uliompita kwa juu kipa huku la pili likiwa mchezo mzuri wa nipa ni kupe kati ya Kolarov.

Manchester United yailaza Benfica ugenini

Kipa Mile Svilar alidondokwa na machozi baada ya kufungwa bao hilo na ikamlazimu M'belgiji mwenzake Lukaku kumnyamazisha

Mkufunzi wa Manchester United Jose Mourinho amesema kuwa sio uhalifu ''kuweka basi'' nyuma huku kikosi chake kikiishinda Benfica katika mechi ya vilabu bingwa Ulaya.

Bao la pekee mjini Lisbon lilifungwa na Marcus Rashford aliyepiga mkwaju wa adhabu na kumwacha kipa wa Benfica Mile Svilar bila jibu.

Svila ambye ni raia wa Ubelgiji na kipa mwenye umri mdogo zaidi aliupangua mpira huo katika goli lake.

Hatahivyo Rashford alikitia wasiwasi kikosi cha United baada ya kutoka nje akiguchia katika kipindi cha pili na mahala pake pakachukuliwa na Anthony Martial.

United walikosolewa kwa mchezo wao katika sare ya 0-0 dhidi ya Liverpool siku ya Jumamosi ambapo walifanya shambulio moja pekee , lakini sasa The Red Devils wamefungwa mabao sita msimuu huu.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz