DAKKA 45 ZA KWANZA : SIMBA 0-1 MTIBWA SUGAR KUTOKA UWANJA WA UHURU - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 15 October 2017

DAKKA 45 ZA KWANZA : SIMBA 0-1 MTIBWA SUGAR KUTOKA UWANJA WA UHURU


Dk 51, basi nzuri sana ya Mohamed Issa lakini Stamili Mbonde anaikosa kidogo tu na kuanguka mwenyewe. Yuko chini anatibiwa

SUB Dk 49 Mbode anatoka kwa upande wa Simba na nafasi yake inachukuliwa na Mganda, Juuko Murshid

Dk 45 Kipindi kimeanza na inaonekaan Simba wanataka kusawazisha lakini Mtibwa wanataka kuongeza bao la pili

MAPUMZIKO

DAKIKA 2 ZA NYONGEZA
Dk 44, Niyonzima anaachia mkwaju wa faulo lakini unakuwa nyanya kabisa kwa kipa
Dk 42 Nyoni anacheza kona nyingine nzuri kabisa hapa, lakini safari Mtibwa Sugar wanaokoa vizuri kabisa
Dk 41, Kotei anaachia mkwaju inakuwa kona, inachongwa wanaokoa tena inakuwa kona
Dk 38, Simba wanaingia vizuri lakini shuti kali la Okwi linapaa juuu
GOOOOOOOOOO Dk 36, kona safi, mabeki wa Simba wakiwa wmazubaa, Mbonde anaruka na kufunga kwa kichwa

GOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOO

Dakika ya 35: Mtibwa wanapata kona mbili mfululizo, Aishi Manula anafanya kazi njzuri kuokoa.

Dakika ya 24: Viungo wa Simba wanaonyesha kuelewana muda mwingi kutokaan na kupigiana pasi.

Dakika ya 24: Viungo wa Simba wanaonyesha kuelewana muda mwingi kutokaan na kupigiana pasi.

Dakika ya 20: Simba wanapiga shuti la mbali lakini mpira unatoka.

Dakika ya 17: Simba wanafanaya mabadiliko, anaingia Juma Liuzio, ametoka Bocco ambaye aliumia mguu.

Dakika ya 13: John Bocco anaumia, amekaa chini, anaonyesha ishara hawezi kuendelea na mchezo, anatolewa nje.

Dakika ya 9: Mtibwa wanalisogelea lango la Simba lakini mpira unaokolewa.

Dakika ya 8: Mkude anapata nafasi ya kupiga pasi nzuri anashangiliwa sana na mashabiki wa timu yake.

Dakika ya 5: Simba wanapata kona, inapigwa lakini inaokolewa.

Dakika ya 2: Mchezo umeanza kwa kasi ya kawaida.

Mwamuzi anaanzisha mchezo.

Huu ni mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

Mchezo unatarajiwa kuanza muda wowote kuanzia sasa, kiungo wa Simba, Jonas Mkude ni mmonja wa wachezaji wanaoanza katika kikosi cha Simba.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment