MOURINHO ATOA YA MOYONI MECHI DHIDI YA LIVERPOOL - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Friday, 13 October 2017

MOURINHO ATOA YA MOYONI MECHI DHIDI YA LIVERPOOL
Meneja wa Manchester United Jose Mourinho amesema litakuwa jambo al kupendeza sana kupeleka klabu yake Anfield Jumamosi licha ya kutarajia kutoshangiliwa.

Klabu hizo mbili ni mahasimu wakuu na United wanaweza kuwa alama 10 mbele ya Liverpool iwapo watashinda mechi hiyo ya Jumamosi.

"Tunajua jinsi mashabiki wao waliovyo na uadui dhidi yetu kihistoria, lakini hilo ndilo tunataka," Mourinho amesema.

"Sijawahi kumuona mchezaji akilalamika 'oh, mazingira yalikuwa mabaya sana'."

"Huwa tunalalamika mashabiki wakiwa kimya. Ni jambo la kupendeza kuchezea Anfield. Jambo la kupendeza sana."


Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atakuwa akiadhimisha miaka miwili Liverpool wikendi hii na atakuwa bila mchezaji wake nyota Sadio Mane.


Mane aliumia misuli ya paja akichezea Senegal mechi za kufuzu Kombe la Dunia lakini Klopp anaamini wanaweza kujimudu bila yeye.


"Bila shaka bado tunaweza kucheza soka bila Sadio kama tulivyofanya awali - zaidi ya jinsi tulivyotaka," amesema Klopp.


"Yeye ndiye mchezaji bora zaidi wetu na ana mkosi sana kuumia.


"Wachezaji wengi wa timu mbalimbali wametoka kuchezea timu za taifa na majeraha - ni tatizo kubwa kutokana na mabadiliko ya mtindo wa mazoezi na uchezaji pia."

"Tunaweza kucheza bila yeye ingawa tungependa sana kuwa na yeye kikosini.
Coutinho kucheza

Liverpool watakuwa bila Mane anayetarajiwa kukaa nje wiki sita, lakini Philippe Coutinho na Roberto Firmino wanatarajiwa kuwepo hata baada ya safari ndefu ya kucheza mechi Brazil.

Kiungo wa kati wa Manchester United Marouane Fellaini anatarajiwa kutocheza baada ya kuumia kano za goti akichezea Ubelgiji.
Nahodha Michael Carrick pia bado anauguza jeraha.

Beki Phil Jones hakuchezea England kutokana na jeraha la goti lakini huenda akacheza Jumamosi.

Mshambuliaji Romelu Lukaku pia yuko sawa kucheza licha ya kutatizwa na kifundo cha mguu karibuni.

Liverpool hawajafanikiwa kuwashinda Manchester United kwa mechi sita Ligi ya Premia tangu ushindi wao wa 3-0 uwanjani Old Trafford Machi 2014 (Sare 2, Kushindwa 4).

United wameshinda mechi tatu kati ya tano za karibuni zaidi walizochezea Anfield (sare 1 na kushindwa 1).

Hawajafungwa bao mechi mbili walizocheza karibuni zaidi. like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment