MATUKIO YOTE YALIYOJIRI MPAMBANO WA SIMBA NA NJOMBE MJI - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 21 October 2017

MATUKIO YOTE YALIYOJIRI MPAMBANO WA SIMBA NA NJOMBE MJIFULL TIME
DAKIKA 4 ZA NYONGEZA
Dk 89, Simba wanaonekana hawana haraka tena, sasa wanakwenda taratibu wakipiga pasi kupoza mpira wakionekana wanawasubiri Yanga katika mechi ijayo
Dk 86, Simba wanapata kona nyingine baada ya krosi safi ya Zimbwe. Inachongwa, Njombe wanaokoa
Dk 85 sasa, Simba wanaonekana kugongeana taratibu kama vile wameridhika na idadi ya mabao hayo manne yyaliyofungwa dakika ya 28, 51, 52 na 58

Dk 84 Gyan anamtoka beki wa Njombe lakini kipa anakuwa mwepesi, anatoka na kuokoa
Dk 82, Njombe wanapata kona, inachongwa lakini Simba wako makini
Dk 75, Nyoni anatolewa nje kwenda kutibiwa
SUB Dk 74 anatoka Muzamiru anaingia Said Ndemla upande wa Simba
KADI Dk 69 kadi ya kwanza ya njano inakwenda kwa ditram Nchimbi baada ya kumuangusha Zimbwe
SUB Dk 68, Njombe wanabadili kipa, Kisu anakwenda kwenye benchi anaingia Mbululo


Dk 64, kipa wa Njombe yuko chini pale anatibiwa. Inawezekana asirudi kwa kuwa ameumia au mwenyewe ameona kuna dalili za nyingi zaidi, hivyo bora kupumzika
Dk 63, Gyan, Niyonzima wanagongeana vizuri na Muzamiru anaachia mkwaju mkali, Kisu anaokoa na kuwa kona, Simba wanachonga lakini hakuna shambulizi kali
Dk 62 Nchimbi anaachia mkwaju mkali hapa lakini Manula anaokoa na kuwa kona, inachongwa, Simba wanaokoa
SUB Dk 61, Nicholas Gyan anaingia kuchukua nafasi ya Mavugo ambaye hivi punde alifunga bao
Dk 60, shambulizi jingine kali la Simba, Njombe wanaokoa na kuwa kona, inachongwa lakini kipa Kisu yuko makini
GOOOOOOOOOOO krosi safi ya Kichuya, Mavugo anaunganisha kwa kichwa na kuwa bao la nne


Dk 57, kiasi fulani wanaonekana kuwa kama wamekata tamaa hivi
Dk 55, pasi nzuri ya Muzamiru, Mkude anaachia mkwaju mkali kabisa hapa, goal kick
GOOOOOOOOO Dk 53 Muzamiru tena, anapokea pasi nzuri ya Okwi aliyeingia vizuri na kuunganisha bao safi kabisa
GOOOOOOOO Dk 51 Muzamiru anaungwanisha krosi nzuri na kuandika basi safi hapa.
Dk 49, krosi nzuri lakini Okwi anaonekana kuhofia kuchomokewa, anaachia shuti juuu
Dk 48, bado hakuna mashambulizi makali na inaonekana mpira unachezwa katikati zaidi
Dk 45 Njombe ndiyo wameuanza mpira na wanaonekana wazi wamepania kusawazisha wakionekana kuwa na kasi


MAPUMZIKO
DAKIKA 1 YA NYONGEZA
Dk 44, Nchimbi anawatoka Juuko na Mlipili, anakwenda yeye akiwa na Manula, anapiga nje, goal kick
Dk 43, Simba wanashambulia mfululizo katika eneo la Njombe lakini wanaonekana kujisahau, mabeki wao hawajipangi vizuri
Dk 41, Okwi anatoa pasi maridadi kwa Mavugo lakini Kisu anakuwa mwepesi kutoka na Mavugo anautoa, goal kick
Dk 40, shuti kali la Muzamiru, kipa Kisu anafanya kazi ya ziada anaokoa


Dk 39, pasi nzuri ya Ditram Nchimbi, Mkude anafanya kazi ya ziada anaokoa na kuwa kona. Inachongwa vizuri hapa, Manula anaokoa na kuwa goal kick
Dk 36, Okwi tena, anaingia vizuri kabisa, anamchambua beki ndani ya 18 lakini anaanguka mwenyewe
Dk 33, Mavugo anawekwa chini hapa, mwamuzi anasema acha kudeka "piga kazi"
Dk 29, Simba wanapata kona nyingine baada ya shambulizi la Simba, inachongwa vizuri lakini ni dhaifu na kipa Kisu anadaka kwa ulaini kabisa
GOOOOOOOO Dk 28, Okwi anaruka juu na kuunganisha vizuri kwa kichwa krosi ya Nyoni, kipa Kisu amaeshika kiuno
Dk 27,Simba wanafanya shambulizi jingine lakini Njombe wako makini. Simba wanashambulia mfululizo na Njombe wanapaswa kuwa makini
Dk 26, pasi nzuri ya Niyonzima,Muzamiru anaachia pasi nzuri kabisa Njombe wanaokoa na kuwa kona, inachongwa vizuri kabisa, Niyonzima anaachia mkwaju mkali hapaa, goal kick


Dk 23, kona ya Niyonzima, Mavugo anapiga kichwa lakini wanaokoa Njombe
Dk 22, Nyoni anaingia na kuachia krosi safi kabisa lakini inakuwa kona
Dk 19, inachongwa kona nyingine safi hapa, Kambole anaruka na kuwazidi ujanja mabeki wa Simba, anapiga kichwa lakini Manula anatokea na kudaka kwa ulaini
Dk 19, Njombe wanachonga kona safi, Juuko anaokoa na kuwa kona ya tatu mfululizo ikiwa ya nne ya Njombe leo
Dk 18, Njombe wanajibu shambulizi, Mlipili anafanya kazi ya ziada kuokoa na kuwa kona. Inachongwa hapa na Manula anaruka juu na kuokoa, kona tena
Dk 17, Simba wanafanya shambulizi jingine zuri baada ya krosi ya Nyoni lakini Kichuya anakuwa si makini


Dk 15 Zimbwe Jr anamtoka mtu na kuingiza krosi ya mkwaju mkali kabisa hapa lakini Njombe wako vizuri, wanaokoa
DK 11, Njombe wanaonekana kuanza kutulia, sasa wanagongeana vizuri wakianza kufunguka kutoka nyuma
Dk 9, kona safi ndani ya lango la Simba lakini Njombe wanacheza faulo
Dk 8, shambulizi kali la Njombe, Juuko anafanya kazi ya ziada kumzuia Bako inakuwa kona ya kwanza ya Njombe
Dk 6 Simba wanafanya shambulizi tena na kupata kona, inachongwa na Kichuya lakini haina madhara
Dk 5 Simba wanafanya shambulizi kali, mkwaju wa Kichuya unaokolewa, Okwi anaachia shuti linaokolewa
Dk 4, Simba wanapata kona ya kwanza lakini kipa David Kisu anadaka kwa ulaini kabisa
Dk 3, Simba wanagongeana vizuri kajuu krosi ya Kichuya inakuwa ni dhaifu
Dk 1, Simba wameanza kwa kasi wanaonekana wamepania kushinda.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment