MANENO YA ZITTO KABWE BAADA YA NYALANDU KUJIUZULU NYADHIFA NDANI YA CCM - EDUSPORTSTZ

Latest

MANENO YA ZITTO KABWE BAADA YA NYALANDU KUJIUZULU NYADHIFA NDANI YA CCM


Maneno ya Zitto Baada ya Nyarandu Kujiuzulu ' Umeonyesha Uongozi, Unahitaji Roho Ngumu Kuwa CCM '
Mbunge wa Kigoma Mjini kwa tiketi ya ACT Wazalendo Zitto Kabwe amefunguka na kumpongeza aliyekuwa Mbunge wa Singida Kaskazini Nyalandu ambaye leo Oktoba 30, 2017 amefanya maamuzi ya kuachana na CCM na kusema kiongozi huyo amefanya maamuzi sahihi.

Zitto Kabwe amesema kuwa kutokana na uchumi unavyoporomoka haki za watu zinavyovunjwa jambo alilofanya Nyalandu ni sawa na kuwa huko ndiyo kuonyesha uongozi.
"Lazaro Nyalandu, umeonyesha Uongozi. Kwa namna haki za watu zinavyovunjwa na Uchumi wa nchi unavyoporomoka, unahitaji roho ngumu Sana kuwa CCM. Umefanya maamuzi sahihi, wakati sahihi na Kwa sababu sahihi. Kila la kheri|" aliandika Zitto Kabwe
Lazaro Nyalandu leo ametangaza kujivua nafasi zake ndani ya Chama Cha Mapinduzi na kuandika barua yake ya kujiuzulu nafasi yake ya Ubunge kwa kile alichodai kuwa Chama Cha Mapinduzi na Bunge vimekuwa vikishindwa kuisimamia serikali na badala yake kutumiwa na serikali jambo ambalo yeye anaona halina afya katika maendeleo ya nchi na linadidimiza haki mbalimbali.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz