MAN UNITED WAILAZA TOTTENHAM HOTSPURS - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 29 October 2017

MAN UNITED WAILAZA TOTTENHAM HOTSPURSMan United yafufuka na kuilaza Tottenham Hotspurs

Bao la kipindi cha lala salama la Anthony Martial's limeiweka Manchester United katika nafasi ya pili katika jedwali la ligi ya Premia baada ya kuilaza Tottenham Hotspurs katika uwanja wa Old Trafford.

Kuingizwa kwa Martial's aliyechukua mahali pake Marcus Rashford baada ya dakika 70 hakukupendelewa na mashabiki wa Man United, lakini meneja Jose Mourinho alionyesha ujasiri wake baada ya mshambuliaji huyo wa Ufaransa kufunga bao ikiwa imesalia dakika tisa pekee kufuatia pasi murua ya Romelu Lukaku.

Ulikuwa ushindi mwembamba wa Man United licha ya kutengeza nafasi chungu nzima katika kipindi cha pili ambapo shambulio la Lukaku liligonga mwamba na jingine kuokolewa na kipa Hugo Lloris.

Spurs ilikosa tisho la ufungaji wa Harry Kane, hivyobasi kutengeza nafasi chache moja ambayo Dele Alli alishindwa na bao la wazi baada ya kupata krosi nzuri kutoka kwa Christian Eriksen.

Mwishowe mabadiliko ya Mourinho na bao zuri la Martial katika eneo hatari yalileta tofauti ya mabao kati ya timu hizo mbili.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment