KICHUYA APATA MKWANJA HUU HAPA BAADA YA KUIFUNGIA SIMBA GOLI - EDUSPORTSTZ

Latest

KICHUYA APATA MKWANJA HUU HAPA BAADA YA KUIFUNGIA SIMBA GOLI


Mashabiki wa Simba kundi la Simba Kwanza (SK) wamekabidhi shilingi 500,000 Shiza Kichuya baada ya kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi ‘Man of the Match’ ikiwa ni kutokana na goli alilowafunga watani wao wa jadi mchezo uliomalizika kwa sare ya kufungana 1-1.

Mashabiki hao wamemchagua Kichuya kuwa Man of the Match wakiwa wameridhishwa na kiwango alichokionesha kwenye mchezo huo.

Kichuya aliifungia Simba bao la kuongoza lakini baadae goli hilo lilisawazishwa na Obrey Chirwa na kulazimisha timu hizo za Kariakoo kugawana pointi.

Mmoja wa viongozi wa kundi hilo amesema, huo utakuwa ni utaratibu wao wa kila mechi kutoa zawadi ya pesa kwa mchezaji atakaefanya vizuri kwenye mechi.

Ameahidi kuwa, mechi ijayo ya Simba (Mbeya City vs Simba November 5, 2017) watatoa kisasi cha shilingi 2,000,000.


 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz