HII NDIO SIRI YA KUTOFUNGA MAGOLI KWA MRISHO NGASSA - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 15 October 2017

HII NDIO SIRI YA KUTOFUNGA MAGOLI KWA MRISHO NGASSA


Ngassa - statistics, analysis, name meaning, list of ...


Tangu kuanza kwa msimu huu Ngassa licha ya kucheza mechi zote tano kabla ya ule wa dhidi ya Mtibwa lakini hajaifungia timu hiyo hata bao moja
Kiungo mshambuliaji wa Mbeya City, Mrisho Ngasa amesema sababu ya kutocheza kwa kiwango chake tangu kuanza kwa msimu huu ni kutokana na ushindani anaopambana nao kutoka was timu pinzani.

Ngassa ameiambia Goal, anatambua kuwa timu yake inamtegemea yeye kutokana na uzoefu aliokuwa nao lakini hilo ndio limekuwa tatizo kubwa la kushindwa kufanya vizuri.

"Nimefanya maandalizi ya kutosha kuweza kufanya vizuri lakini mambo yamekuwa tofauti kwani msimu huu ushindani umeongezeka na hilo limechangia nishindwe kuisaidia timu yangu," amesema Ngassa.


Mchezaji huyo wa zamani wa Yanga amesema pamoja na changamoto zote anazokumbana nazo lakini anafurahi kuona wachezaji wenzake wakiendelea kumwakilisha vizuri na kuiweka timu hiyo kwenye nafasi nzuri kiasi.

Ngassa amesema sare na ushindi wanaopata katika baadhi ya mechi zimekuwa zikimpa matumaini ya kufanya vizuri endapo atatulia na kujipanga kwa ajili ya kupandisha kiwango chake kwenye kikosi cha Simba.

Tangu kuanza kwa msimu huu Ngassa licha ya kucheza mechi zote tano kabla ya ule wa dhidi ya Mtibwa lakini hajaifungia timu hiyo hata bao moja.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment