HII NDIO REKODI INAYOFUKUZIWA NA MAN UNITED PAMOJA NA MAN -CITY LEO - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 21 October 2017

HII NDIO REKODI INAYOFUKUZIWA NA MAN UNITED PAMOJA NA MAN -CITY LEO


Tarehe 18 September mwaka 1999 ndio ilikuwa mara ya mwisho wa Watford kuwafunga
Chelsea, lakini mwezi May mwaka 1986 ilikuwa mara ya mwisho kwa Watford kupata ushindi katika dimba la Stamford Bridge.
Katika michezo 10 iliyopita kati ya Watford na Chelsea, Watford wameambulia suluhu mbili tu huku michezo nane iliyobaki wakichezea kipigo lakini Chelsea nao wameshindwa kupata hata pointi moja katika michezo yao miwili iliyopita ya Epl.
Manchester United nao hii leo watakuwa katika dimba la John Smith kukabiliana na Huddersfield huku wenyeji wakiwa na kumbukumbu ya miaka 46 iliyopita walipowakaribisha United na kuchezea kipigo cha bao 3.
United wanaingia katika mchezo huu wakiwa na rekodi nzuri sana msimu huu ambapo wakishinda wataweka rekodi ya kupata alama 23 ndani ya michezo 9 ya mwanzo ya ligi kuu huku wapinzani wao hawajashinda katika mechi 6 zilizopita.
Manchester City wanakutana na Burnley ambapo City katika mechi zake zilizopita dhidi ya Burnley waneshindwa kutoruhus kufungwa goli lakini Burnley wakipata ushindi mara moja tu dhidi ya City katika mechi 16 zilizopita.
Manchester City wakishinda katika mchezo wa leo wataweka rekodi mpya ndani ya klabu hiyo, rekodi ya kushinda michezo 11 mfululizo katika mashindano yote na watakuwa wameshinda michezo 7 mfululizo katika ligi kuu.
Katika mchezo mwingine Newcastle watacheza dhidi ya Crystal Palace, Swansea watawakaribisha Leicester City, Southampton dhidi ya West Bromich Albion na Fc Bournamouth watawafuata Stoke City.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment