HAYA YOTE YAMEFANYWA NA SAMATTA AKIWA NA KRC GENK MPAKA SASA - EDUSPORTSTZ

Latest

HAYA YOTE YAMEFANYWA NA SAMATTA AKIWA NA KRC GENK MPAKA SASA




MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta jana amecheza mechi yake ya
69, timu yake, KRC Genk ikilazimisha sare ya 0-0 na wenyeji, KV Kortrijk katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A, Ubelgiji uliofanyika Uwanja wa Guldensporen mjini Kortrijk.

Samatta alicheza kwa dakika 70 kabla ya kumpisha Nikolaos Karelis aliyekuwa anarejea uwanjani kwa mara ya kwanza baada ya kuwa nje kwa muda mrefu kutokana na kuwa majeruhi.

Katika mechi hizo 69, Samatta, mshambuliaji wa zamani wa Mbagala Market, African Lyon na Simba za Tanzania, amefunga mabao 22 kwenye mechi za mashindano yote tangu alipowasili Genk Januari mwaka jana akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).

Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika mwaka jana alipokuwa na Mazembe, 41 ameanza na mechi 24 ametokea benchi.

Kikosi cha KV Kortrijk kilikuwa: Kaminski, Verboom, Kovacevic, Rougeaux, Attal, D'Haene/Kagé dk84, Vanderbruggen, Azouni, Ajagun, Chevalier and Perbet/Budkivskyi dk72.

KRC Genk : Vukovic, Uronen, Colley, Aidoo, Mata/Maehle dk74, Heynen, Writers, Malinovskyi/Buffalo dk87, Pozuelo, Samatta/Karelis dk70 na Ingvartsen.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz