DONDOO NA STORI ZA SOKA KWA NCHI AMBAZO TIARI ZIMEFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2018 - EDUSPORTSTZ

Latest

DONDOO NA STORI ZA SOKA KWA NCHI AMBAZO TIARI ZIMEFUZU KUSHIRIKI KOMBE LA DUNIA 2018

Mshambuliaji wa Paris St-Germain Neymar ndiye mchezaji ghali zaidi duniani

AMERIKA KUSINI
Brazil

Ustadi: Washindi mwaka 1958, 1962, 1970, 1994 na 2002, Brazil walilazwa 7-1 hatua ya makundi na Ujerumamni mwaka 2014.

Mchezaji nyota: Neymar. Alinunuliwa £200m na Paris St-Germain na amekuwa akifunga bao na kusaidia kila mechi tangu wakati huo. Pele amesema Neymar, 25, ndiye mchezaji bora zaidi wa taifa hilo na anaamini atashinda Ballon d'Or.

Wachezaji Ligi ya Premia: Ederson, Fernandinho, Gabriel Jesus (wote wa Manchester City), Philippe Coutinho, Roberto Firmino (wa Liverpool), Willian (Chelsea).

Mkufunzi? Tite alichukua nafasi ya Dunga wakiwa nafasi ya sita, theluthi ya mechi za kufuzu zikiwa zimechezwa. Lakini mkufunzi huyo wa zamani wa Corinthians, 56, amewasaidia kuwa alama 11 mbele ya Colombia kileleni zikiwa zimesalia mechi tatu.

AMERIKA KASKAZINI NA KATI na CARIBBEAN
Mexico

Ustadi: Mexico wamefika hatua ya muondoano kila michuano ya Kombe la Dunia sita iliyochezwa. Walifika robofainali wakiwa wenyeji mwaka 1986.

Mchezaji nyota: Hirving Lozano amefunga mabao matatu mechi tatu kati aihame Pachuca na kwenda PSV Eindhoven majira ya joto.

Lozano, 22, ameanza kuwa nyota timu ya taifa ambapo alifunga bao la ushindi dhidi ya Panama.

Alimpendeza hata Diego Maradona akicheza mechi yake ya kwanza Eredivisie.

Wachezaji Ligi ya Premia: Javier Hernandez (West Ham).

Mkufunzi? Meneja msaidizi wa zamani waManchester City Juan Carlos Osorio ndiye anayewaongoza. Alikuwa awali amepigwa marufuku mechi sita na Fifa kwa kumtusi mwamuzi Kombe la Mabara. Ni raia wa Colombia aliyesomea stashahada ya sayansi na soka kutoka chuo kikuu cha John Moores cha Liverpool.
Costa Rica

Ustadi: Urusi 2018 itakuwa mara ya tano kwa Los Ticos kucheza michuano ya Kombe la Dunia.

Brazil walimaliza kileleni mwa kundi lililokuwa na Uruguay, Italia, na England. Waliondolewa robofainali kwa mikwaju ya penalti na Uholanzi.

Mchezaji nyota: Beki wa Bologna Giancarlo Gonzalez alikuwa kwenye kikosi bora cha wachanganuzi wa BBC wa Kombe la Dunia mwaka 2014 lakini ufanisi wa sasa wa Costa Rica unatokana na kipa Keylor Navas, 30. Alicheza vyema sana 2014 kiasi cha Real Madrid kumnunua na sasa ndiye kipa wao nambari wani.

Ameshinda La Liga na makombe mawili ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.

Wachezaji Ligi ya Premia: Joel Campbell wa Arsenal ambaye yuko kwa mkopo Real Betis.

Mkufunzi? Oscar Ramirez ambaye alikuwa mchezaji Costa Rica walipocheza Kombe la Dunia mara ya kwanza 1990. Alichukua usukani 2015 baada ya Paulo Wanchope kujiuzulu.
ASIA
Iran

Ustadi: Ni mara ya tano Iran kufuzu Kombe la Dunia.

Mechi pekee waliyoshinda ni 2-1 dhidi ya Marekani michuano ya Ufaransa '98.

Mchezaji nyota: Mshambuliaji Sardar Azmoun ambaye kimsingi ndiye mshambuliaji bora zaidi Asia baada ya raia mwenzake Ali Daei, ambaye amefunga mabao mengi kimataifa kuzidi mchezaji mwingine yeyote wa kiume. Azmoun, 22, ni stadi sana kwa miguu na kwa kichwa. Huchezea Rubin Kazan ya Urusi.

Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja

Mkufunzi? Carlos Queiroz amekuwa mkufunzi kwa muda mrefu na ana tawasifu ya kupendeza. Amukuwa mkufunzi Sporting Lisbon, Afrika Kusini, Real Madrid na alikuwa msaidi wa Sir Alex Ferguson Manchester United.

Na amehudumu mara mbili Ureno.

Amekuwa mkufunzi wa Iran kwa miaka sita iliyopita.
Japan

Ustadi: Wameshiriki tangu 1998, Japan na walipita hatua ya makundi mara mbili, ikiwa ni pamoja na 2002 walipokuwa wenyeji wenza na Korea Kusini.

Mchezaji nyota: Keisuke Honda, Shinji Kagawa na nyota wa Leicester Shinji Okazaki wamekuwa wachezaji nyota. Lakini kuna kinda wa Arsenal Takuma Asano ambaye tayari amefungia cnhi yake mechi tatu na alisaidia Stuttgart kupanda daraja Bundesliga msimu uliopita akiwa kwa mkono kutoka kwa Gunners. Wenger amemweleza kama mshambuliaji mwenye kipaji na mwenye matumaini siku za usoni.

Wachezaji Ligi ya Premia: Maya Yoshida (Southampton), Shinji Okazaki (Leicester City), Takuma Asano (Stuttgart, kwa mkopo kutoka Arsenal).

Mkufunzi? Vahid Halilhodzic, ingawa huenda akaondoka kwani kuna fununu kuhusu mzozo kwenye timu.

Aliongoza Algeria kufika hatua ya muondoano mara ya kwanza 2014.

Ni mchezaji wa zamani wa Yugoslavia ambaye amewahi kuwa mkufunzi wa Paris St-Germain, Dinamo Zagreb na Ivory Coast.
Saudi Arabia

Ustadi: Saudi Arabia walishinda mechi zao pekee Kombe la Dunia mara yao ya kwanza 1994, waliposhinda mechi mbili za hatua ya makundi na kufika raundi ya pili.

Ushindi wao mechi ya pili, 1-0 dhidi ya Ubelgiji, ulitokana na moja ya mabao yanayokumbukwa zaidi - Saeed Al Owairan alipokimbia kutoka nusu yao ya uwanja na kuwachenga nusu ya walinzi wa Ubelgiji kisha kufunga.

Mchezaji nyota: Mshambuliaji mkongwe Nasser Al Shamrani atakuwa na mchango muhimu.

Ni mchezaji bora wa mwaka Asia mwaka 2014.

Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja

Mkufunzi? Bert van Marwijk, ambaye amekuwa kwenye usukani tangu 2015. Mholanzi huyo wa miaka 65, aliwaongoza Uholanzi kufika fainali Kombe la Dunia 2010. Amekuwa pia mkufunzi wa Borussia Dortmund, Feyenoord na Hamburg.

Korea Kusini

Ustadi:Ndiyo timu ya Asia yenye rekodi nzuri. Hufahamika kwa jina la utani Mashujaa wa Taegeuk. Walifuzu kwa michuano yao ya 10 kwa sare dhidi ya Uzbekistan. Urusi itakwua mara yao ya tisa mtawalia kushiriki.

Mchezaji nyota: Son Heung-min alionyesha ustadi wake Tottenham. Hata hivyo, amefunga bao moja pekee kimataifa tangu 2016. Mfuatilie zaidi Lee Dong-gook aliyeingia kama nguvu mpya mechi yao ya mwisho ya kufuzu na ambaye atakuwa na miaka 39 michuano ikianza mwaka ujao. Ni mshambuliaji wa zamani wa Middlesbrough ambaye amechezea timu ya taifa mechi 105 miaka 19.

Wachezaji Ligi ya Premia: Ki Sung-yueng (Swansea), Son Heung-min (Tottenham)

Mkufunzi? Shin Tae-yong ambaye amepewa jina la utani 'Mourinho wa Asia' amekumbwa na shinikizo kutokana na kutofanikiwa sana mechi za kufuzu. Hata hivyo, alichukua usukani Julai na huenda akapewa muda zaidi. Ana miaka 48 na alicheza Ligi Kuu ya Korea Kusini miaka 12 na mechi moja ligi kuu Australia kabla ya kustaafu 2005.

AFRIKA
Misri

Ustadi: Misri wamo nafasi ya 30 orodha ya Fifa, moja chini ya Uholanzi. Hawakufuzu michuano ya 2010 na 2014 baada ya kushindwa mechi za muondoano za kufuzu baada ya hatua ya makundi.

Wamefuzu kwa bao la ushindi kutoka kwa Mohamed Salah wa Liverpool dhidi ya Congo 8 Oktoba.

Ufanisi wao mkubwa karibuni ni mwaka 2010 waliposhinda Kombe la Mataifa ya Afrika mara yao ya saba.
Mchezaji nyota: Mohamed Salah, aliyenunuliwa na Liverpool majira ya joto, ndiye mchezaji mwenye kipaji zaidi Misri. Ana kasi sana na amefunga mabao 32 mechi 56 za kimataifa, zikiwemo tano mechi za kufuzu kwa Urusi.

Wachezaji Ligi ya Premia: Mohamed Salah (Liverpool), Mohamed Elneny (Arsenal), Ahmed Hegazy (West Brom), Ramadan Sobhi (Stoke),

Wachezaji Championship: Ahmed Elmohamady (Aston Villa)

Wachezaji League One: Sam Morsy (Wigan),

Mkufunzi? Raia wa Argentina Hector Cuper, ambaye amewahi kuwa mkufunzi waValencia na Inter Milan, alichaguliwa kuwa mkufunzi mkuu Machi 2015.

Alikuwa pia mkufunzi wa Georgia kati ya 2008 na 2009.

Michuano yake mikubwa kuongoza timu ilikuwa Kombe la Mataifa ya Afrika 2017 ambapo Misri walilazwa 2-1 kwenye fainali na Cameroon.
Nigeria

Ustadi: Hii itakuwa mara ya sita kwa Nigeria kushiriki fainali za Kombe la Dunia, ma mara yao ya tatu mtawalia.

Wamefika hatua ya 16 bora mara tatu - 1994, 1998 na 2014 - lakini hawajawahi kupita hatua hiyo.

Mchezaji nyota: Nahodha wao John Mikel Obi, ndiye mchezaji wao mwenye uzoefu zaidi kikosini, ambapo amechezea taifa mechi 80 na atakuwa nguzo muhimu katika kikosi cha Super Eagles Kombe la DUnia Urusi.

Itakuwa mara ya pili kwa mchezaji huyo wa zamani wa Chelsea kushiriki michuano hiyo.

Mikel, 30, aliwasaidia kufika hatua ya muondoano 2014 kwa mara ya kwanza tangu 1998.

Kwa sasa yeye huchezea klabu ya Tianjin Teda ya China.

Wachezaji Ligi ya Premia: Alex Iwobi (Arsenal), Victor Moses (Chelsea), Kelechi Iheanacho (Leicester City), Wilfred Ndidi (Leicester City), Ahmed Musa (Leicester City) na Ola Aina (kwa mkopo Hull City kutoka Chelsea).

Mkufunzi? Gernot Rohr ambaye amefanya kazi ya ukufunzi nchi nyingi duniani ndiye mkufunzi wao kwa sasa.

Amewahi kuwa mkufunzi Nice hadi Gabon, Burkina Faso hadi Nigeria.

Mjerumani huyo wa miaka 64 ana tajriba ya hali ya juu.

Rohr alichezea Bayern Munich na Bordeaux.

Kisha alikuwa mkufunzi wa Bordeaux waliposhindwa fainali ya Kombe la Uefa mwaka 1996 na Bayern.

Klabu alizowahi kuwa mkufunzi ni pamoja na Nantes ya Ufaransa, Young Boys Berneya Uswizi, Etoile du Sahel na pia amewahi kuwa mkufunzi Niger.

Michuano ya mwisho ya hatua za makundi kufuzu kwa Kombe la Dunia nchini Urusi mwaka ujao inaendelea kufanyika. Kwa sasa mataifa 14 tayari yamejikatia tiketi kushiriki michuano hiyo itakayoshirikisha nchi 32 mwaka ujao.

Mabingwa mara tano Brazil wamefuzu, sawa na mabingwa watetezi Ujerumani, pamoja naIceland, Ubelgiji, Costa Rica, England, Misri, Iran, Japan, Mexico, Nigeria, Poland, Saudi Arabia,Serbia, Korea Kusini na Uhispania.

Walifikaje huko? Nani wachezaji wao nyota? Na wakufunzi waliowafikisha huko?
ULAYA

Urusi (wenyeji)

Ustadi: Vijana hao chini ya Stanislav Cherchesov watakiwa timu ya nne kutoka Urusi kucheza Kombe la Dunia. Mara ya kwanza walishiriki Marekani '94 - ingawa Muungano wa Usovieti ulimaliza nambari nne mwaka 1966.

Ndio wenyeji
Kikosi chote cha wachezaji wa Urusi waliocheza Kombe la Mabara mwaka 2017 Urusi walikuwa wanachezea klabu za nyumbani


Mchezaji nyota: Kipa wao mkongwe Igor Akinfeev amechezea nchi hiyo zaidi ya mechi 100 na uzoefu wake utakwua muhimu.

Akinfeev, 31, amechezea CSKA Moscow maisha yake yote ya uchezaji soka ya kulipwa. Huenda akawa nahodha wa Urusi.

Wachezaji Ligi ya Premia: Hawana hata mmoja.

Mkufunzi? Cherchesov ni kipa wa zamani wa timu ya taifa ya Muungano wa Usovieti na Urusi. Lengo lake ni kuwafikisha nusu fainali.
Ubelgiji

Ustadi: Hawakufuzu kwa michuano miwili iliyotangulia lakini Brazil 2014 walifika robofainali, ambapo waliondolewa na Argentina. Mwaka 1986 walimaliza wa nne.

Wachezaji Ligi ya Premia: Michy Batshuayi, Thibaut Courtois, Eden Hazard (wote wa Chelsea), Simon Mignolet (Liverpool), Toby Alderweireld, Moussa Dembele, Jan Vertonghen, (wote wa Tottenham), Kevin de Bruyne, Vincent Kompany (wa Manchester City), Marouane Fellaini, Romelu Lukaku (wa Manchester United), Steven Defour (Burnley), Nacer Chadli (West Brom), Kevin Mirallas (Everton), Christian Benteke (Crystal Palace), Divock Origi (Wolfsburg, kwa mkopo kutoka Liverpool), Christian Kabasele (Watford).

Mkufunzi? Roberto Martinez aliyesaidia Wigan kushinda Kombe la FA mwaka 2013
England

Ustadi: Tangu waliposhinda Kombe la Dunia 1966, England wamefika nusu fainali mara moja pekee - mwaka 1990, ambapo walimaliza wa nne. Miaka minne iliyopita, waliondolewa hatua ya makundi. Ilikuwa mara yao ya mwisho kukosa kupita hatua ya makundi tangu 1958.

Mchezaji nyota: Harry Kane amefunga magoli 13 akichezea klabu ya taifa Septemba na kwa sasa ni miongoni mwa washambuliaji wanaofunga mabao sana. Mwaka 2017 amefunga mabao 27 ambapo amepitwa tu na Lionel Messi, anayemzidi kwa magoli tisa.

Wachezaji Ligi ya Premia: Kikosi chote cha England hucheza EPL

Mkufunzi? Gareth Southgate anaongoza timu kwa mara ya kwanza katika michuano mikubwa.
Ujerumani

Ustadi: Ni mabingwa watetezi, wameshinda Kombe la Dunia mara nne na wameorodheshwa kuwa timu bora zaidi duniani na Fifa kwa sasa.

Mchezaji nyota: Toni Kroos. Kando na Thomas Muller na Mesut Ozil, kiungo huyo wa Real Madrid ndiye mchezaji mzoefu zaidi kwenye kikosi.

Alikuwa kwenye kikosi kilichoshinda Kombe la Dunia 2014, ameshinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya mara mbili, La Liga mara moja na Kombe la Dunia la Klabu mara mbili.

Wachezaji Ligi ya Premia: Shkodran Mustafi (Arsenal), Antonio Rudiger (Chelsea), Emre Can (Liverpool), Ilkay Gundogan (Manchester City), Mesut Ozil (Arsenal), Leroy Sane (Manchester City).

Meneja? Joachim Low. Alikuwa mkufunzi msaidizi wa Jurgen Klinsmann 2004 hadi 2006, alipochukua hatamu. Aliwaongoza kushinda Kombe la Dunia mwaka 2014 na pia alishinda Kombe la Mabara mwaka huu. Hata hivyo hajashinda Euro. Walimaliza wa pili mwaka 2008 na nafasi ya tatu 2012.
Iceland

Ustadi: Iceland watakuwa wanashiriki Kombe la Dunia wka mara ya kwanza kabisa baada ya ushindi wao dhidi ya Kosovo tarehe 9 Oktoba kuwahakikishia nafasi.

Wamekuwa wakifanikiwa sana karibuni. Walifika Euro 2016, na kulaza England raundi ya pili kabla ya kulazwa 5-2 na wenyeji katika robofainali.

Mchezaji muhimu: Ni vigumu kumtazama mchezaji mwingine ila Gylfi Sigurdsson wa Everton. Mchezaji huyo wa miaka 28 aliwafungia bao la kwanza dhidi ya Kosovo na ni mshambuliaji hatari sana, hasa kwa makombora ya mbali.

Wachezaji wa Ligi ya PremiaGylfi Sigurdsson (Everton), Johann Berg Gudmundsson (Burnley).

Wachezaji Championship: Birkir Bjarnason (Aston Villa), Horour Bjorgvin Magnusson (Bristol City), Jon Dadi Bodvarsson (Reading).

Mkufunzi? Heimir Hallgrimsson, 50, ni daktari wa meno aliyekuwa anasimamia timu hiyo kwa pamoja na Lars Largerback wa Sweden wakati wa michuano ya ubingwa Ulaya nchini Ufaransa. Hallgrimsson alichukua usukani kamili baada ya Euro 2016 na kuwasaidia kufana mechi za kufuzu.
Poland

Ustadi: Poland wameorodheshwa wa sita duniani. Hawajawahi kushinda Kombe la Dunia lakini mwaka huu wanaamini wana kikosi stadi zaidi. Ufanisi wao awali ulikuwa kumaliza nafasi ya tatu, mwaka 1974 na 1982.

Mchezaji nyota: Mshambuliaji wa Bayern Munich Robert Lewandowski amefunga mabao 16 katika mechi tisa za kufuzu Kombe la Dunia akiwa na Poland. Anashikilia nafasi ya tatu kufunga mabao mengi historia ya Poland. Ndiye nahodha na amefunga mabao 51 mechi 91 za kimataifa.

Wachezaji Ligi ya Premia: Lukasz Fabianski (Swansea), Grzegorz Krychowiak (West Bromwich Albion), Kamil Grosicki (Hull City)

Wachezaji Championship: Pawel Wszolek (Queens Park Rangers)

Mkufunzi? Adam Nawalka amewaongoza tangu Novemba 2013 mechi 39. Mkataba wake unafika mwisho Desemba lakini aliwafikisha robo fainali Euro 2016, miaka miwili baada yao kushindwa kufuzu Kombe la Dunia 2014.
Serbia

Ustadi: Mwaka ujao itakuwa mara ya 12 kwa Serbia kucheza Kombe la Dunia. Hawakufanikiwa kupita hatua ya makundi mwaka 2006 na 2010.

Mchezaji nyota: Branislav Ivanovic anakaribia kuchezea taifa lake mechi 100 na ni mchezaji muhimu sana kwao. Ndiye nahodha na kiongozi.

Wachezaji Ligi ya Premia: Nemanja Matic (Manchester United), Aleksandar Mitrovic (Newcastle), Lazar Markovic (Liverpool), Dusan Tadic (Southampton).

Mkufunzi? Slavoljub Muslin, aliyeteuliwa Mei 2016, ni mkufunzi ambaye amesafiri kwingi. Anafanya kazi ya kuwa mkufunzi wa timu ya taifa mara ya kwanza na hajawahi kuongoza timu katika michuano mikubwa. Lakini amefanikiwa ligini Bulgaria.
Uhispania

Ustadi: Wameorodheshwa 11 duniani. Walikuwa namba moja duniani kuanzia 2008 hadi 2013.

Walikuwa mabingwa wa dunia 2010 na mabingwa wa Ulaya 2008 na 2012.

Mchezaji nyota: Kiungo wa kati mshambululiaji wa Real Madrid Isco amekuwa kwenye fomu nzuri sana mechi za kufuzu. Amefunga mabao sita mechi saba za karibuni zaidi za Uhispania. Amefunga mabao saba mechi 23 za kimataifa.

Wachezaji Ligi ya Premia: Juan Mata (Manchester United), Nacho Monreal (Arsenal), Alvaro Morata (Chelsea), David de Gea (Manchester United), Cesar Azpilicueta (Chelsea), Ander Herrera (Manchester United), Pedro (Chelsea), David Silva (Manchester City).

Mkufunzi? Julen Lopetegui aliteuliwa Julai 2016 na hajashindwa mechi 13 ambazo amewaongoza.
 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI










Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz