BILA KITITA HIKI TOTTENHAM HOTSPUR HAIJAMUUZA HARRY KANE - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Tuesday, 17 October 2017

BILA KITITA HIKI TOTTENHAM HOTSPUR HAIJAMUUZA HARRY KANE

Harry Kane

Imeripotiwa kuwa Tottenham Hotspur haitakuwa tayari kumuuza Harry Kane kwa ada ya chini ya paundi milion 200.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 24 amekuwa akivipamba vichwa vingi vya habari kwa siku za hivi karibuni kutokana na uwezo wake mkubwa wa kufumania nyavu.

Baada ya kushindwa kufunga lolote mwezi Agosti, Kane alifunga mabao 11 mnamo Septemba, ambayo pamoja na mabao matatu pekee'dhidi ya APOEL katika Ligi ya Mabingwa.

Fomu ya mshambuliaji huyo inaaminika kuwa imewavutia Real Madrid, na ripoti za hivi karibuni zinasema kuwa klabu hiyo iko tayari kuwajumuisha Gareth Bale, Karim Benzema na Luka Modric kwenye dili hilo.


Kwa mujibu wa Times, mwenyekiti wa Tottenham Daniel Levy amepanga kumbakisha nyota huyo kwenye kikosi cha mwalimu Mauricio Pochettino, kama kuna klabu itamuhitaji basi iweke paundi millioni 200 kwenye kichwa cha Kane.

Neymar ndiye mchezaji wa ghali zaidi katika historia kwa sasa alisajiliwa na Paris Saint-Germain akitokea Barcelona wakati wa majira ya joto katika mkataba wa thamani ya karibu paundi millioni 195.

Kane amekuwa sehemu ya Spurs tangu mwaka 2004 alipojiunga na akademia yao akitokea Watford.
like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment