USICHOKIJUA KUHUSU WILLY SAGNOL KOCHA MRITHI WA CARLO ANCELOTTI BAYERN MUNICH - EDUSPORTSTZ

Latest

USICHOKIJUA KUHUSU WILLY SAGNOL KOCHA MRITHI WA CARLO ANCELOTTI BAYERN MUNICH



 KOCHA  MPYA BARYAN MUNICH
Tofauti na wengi walivyodhani kwamba Bayern Munich eakimuondoa tu Ancelotti watampa kazi kocha mwingine mwenye jina kubwa lakini wameamua kumpa timu kwa muda Willy Sagnol ambaye pia matokeo yanaweza kuamua nafasi yake.

Pamoja na kutumia muda wake mwingi wa soka katika nchi ya Ujerumani lakini Sagnol sio Mjerumani, Sagnol ni raia wa Ufaransa na alizaliwa Ufaransa katika jiji la Ettiene, hiyo ilikuwa mwaka 1977.

Sagnol katikati ya mwaka 2002 na 2009 aliitumikia Bayern Munich katika michezo zaido ya 180 huku akifanikiwa kubeba makombe 10 na klabu hiyo, ni wazi kwamba anaijua vyema Bayern na anajua utamaduni wa klabu hiyo.

Mwaka 2008 Sagnol aliingia katika vichwa vya habari nchini Ujerumani baada ya ugomvi mkubwa kati yake na kocha wa Bayern Munich kipindi hicho Ottmar Hitzfield ugomvi uliopelekea Sagnol kutoswa katika kikosi cha Bayern kilichosafiri kwenda kucheza na St Petersburg.

Sagnol mwaka 2000 pia aliingia katika mzozo na klabu ya Ufaransa ya Monaco kuhusu maslahi baada ya Sagnol kudai ya kwamba Monaco walikuwa wakimlipa kiasi kidogo sana cha pesa na kumuona mjinga kwa kuwa alikuwa na umri mdogo kitu kilichomfanya kuachana nao.

Sagnol ambaye kwa mashabiki wa Bayern anafahamika kama “The God Of Cross” aliwahi kuifundisha klabu ya Ligue 1 ya Bordeaux lakini pia amewahi kuifundisha timu ya taifa ya Ufaransa chini ya miaka 21 na baada ya uwepo wake katila benchi la ufundi la Bayern Munich sasa anakwenda kuwa kocha mkuu.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>



CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI






Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz