SIMBA NA AZAM FC WATUNISHANA MISURI UWANZA WA CHAMAZI - EDUSPORTSTZ

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Saturday, 9 September 2017

SIMBA NA AZAM FC WATUNISHANA MISURI UWANZA WA CHAMAZI


Timu ya Simba imeshindwa kuonyesha ubabe wake mbele ya wana 'lambalamba' Azam Fc, kwa kutoka bila bila kwenye game yao ya leo iliyofanyika nyumbani kwa Azam Fc uwanja wa Chamazi.

Mchezo huo wa Ligi Kuu Soka Tanzania Bara ni wa pili kwa timu ya Simba ambayo mpaka sasa ndio inaongoza kwenye msimamo wa ligi kwa kuwa na point 4 na magoli 7, ikijumlishwa na moja ya leo ambayo wamegawana na timu ya Azam kwa kutoa sare.

Akizungumza mara baada ya mchezo huo mchezaji wa Azam Himid Mao ambao nao wameshindwa kujitunisha misuli kwa mnyama SImba, amesema mchezo ulikuwa mgumu kwa timu zote mbili.

"Kutoka sare sio kitu kizuri ingawa matokeo yalistahili kwa timu zote mbili, mchezo ulikuwa mgumu lakini kila timu ilicheza vizuri, tunawashukuru mashabiki na wadau waliokuja kutusuport", alisema Himid Mao.

Pamoja na mechi hiyo katika uwanja wa Sokoine Mbeya timu ya prisons imemaliza mchezo wake kwa kutoka sare ya magoli 2-2dhidi ya Majimaji ya Songea.like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment