BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 24 September 2017

SAMATTA ASHIDWA KUONESHA UBABE WAKE GENK SAMATTAMbwana Samatta ameanza kwa uzito msimu huu kutokana na kushindwa kuendeleza wimbi la kufunga magoli kama alivyokuwa akifanya msimu uliopita


Mshambulaji wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta alikuwemo dimbani Jumamosi, katika uwanja wa Luminus Arena mjini Genk kwa dakika zote, timu yake, KRC Genk ikilazimishwa sare ya 1-1 na KV Oostende katika mchezo wa Ligi Daraja la Kwanza A Ubelgiji.

Kiungo wa kimataifa wa Ukraine, Ruslan Malinovskiy alianza kuifungia Genk dakika ya 44, kabla ya mshambuliaji Mbelgiji, Zinho Gano kuisawazishia KV Oostende dakika ya 74.

Huo unakuwa mchezo wa 64 kwa Samatta katika mashindano tangu Januari 2016 alipojiunga na Genk, akitokea TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC).


Katika mechi hizo, Samatta ambaye ni mshindi wa tuzo ya Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika 2016 alipokuwa na Mazembe, 37 alianza na mechi 24 alitokea benchi.

Katika mechi hizo, mshambuliaji huyo amefunga jumla ya mabao 21 kwenye mashindano yote.

like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment