JEZI YA TSHISHIMBI KUPOKELEWA KWA SALUTI NJOMBE - EDUSPORTSTZ

Latest

JEZI YA TSHISHIMBI KUPOKELEWA KWA SALUTI NJOMBE




Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.

JEZI za kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi tayari zimeanza kuuzwa kwa kiwango cha juu mkoani Njombe ikiwa ni siku chache kabla ya Yanga haijacheza na Njombe Mji kwenye Uwanja wa Sabasaba mkoani humo.

Njombe Mji na Yanga zinatarajiwa kupambana keshokutwa Jumapili ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara ambapo Tshishimbi tayari ameshajizolea umaarufu kutokana na kiwango kikubwa alichokionyesha kwenye mechi yake ya kwanza hapa nchini dhidi ya Simba katika Ngao ya Jamii.


Licha ya kuwepo kwa jezi nyingi za wachezaji mbalimbali wa Yanga, lakini zenye jina la Tshishimbi raia wa DR Congo, ndizo zilikuwa nyingi huku ikisemekana kwamba ndizo zilizokuwa zikinunuliwa kwa wingi.


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz