BARCELONA KINARA WA KUVUNJA REKODI ZAKE YENYEWE - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Sunday, 24 September 2017

BARCELONA KINARA WA KUVUNJA REKODI ZAKE YENYEWE


 BARCELENO KATIKA RECODI

Kikosi cha Ernesto Valverde kimepata ushindi mnono ugenini dhidi ya Girona wakiwa wameruhusu magoli mawili tu msimu wote

Mwanzo mzuri wa msimu kwa Barcelona unaendelea. Vijana wa Valverde wakiinyuka Girona 3-0 katika mechi ya kihistoria, mechi kubwa ya Catalan kwenye La Liga baada ya mashabiki wote kupiga kura kudai uhuru wa Catalan kutoka Hispania, ni Blaugrana waliojitenga dhidi ya timu zote za Primera Division kwa pengo kubwa la alama 18.

Ushindi huo ni neema kubwa kwa Barcelona, ambapo mabao mawili ya mwanzo ni magoli ya kujifunga kutoka kwa Aday Benitez (aliyekutana na shuti la Jordi Alba) na mlinda mlango Gorka Iraizoz (aliyekumbana na krosi ya Aleix Vidal na kujifunga mwenyewe), kabla ya Luis Suarez kufunga goli la tatu.

Kiwango kikubwa kutoka kwa kikosi cha Valverde na kumaliza mechi nyingine bila kuruhusu goli. Barca wameruhusu goli mara mbili tu msimu huu kwenye La Liga 2017-18 na rekodi hiyo inafanana na rekodi yao nyingine ya 2001-02. Timu moja tu kutoka Ligi Kuu tano bora za Ulaya, Borussia Dortmund imeruhusu magoli machache kwenye ligi msimu huu.

Ikiwa kulikuwa na alama ya kiulizo kuhusu Valverde, ni namna gani timu yake ingeweza kufanya vizuri mechi za ugenini, kwani Athletic Club ilishindwa kufanya vizuri mara kadhaa ugenini. Na ni kweli kwamba Barcelona haina historia ya kufanya vizuri nje ya uwanja wa Camp Nou (Ambao utatimiza mwaka wa 60 Jumapili) katika kampeni hizi.

Lakini mambo ni mswano. Mechi ya kwanza ya Barca ugenini ilikuwa ushindi wa 2-0 dhidi ya Alaves, kabla ya vita kali ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Getafe wikiendi iliyopita na sasa ushindi wa 3-0. Soka safi halina uhakia wa kushinda mataji, lakini umahiri na kufunga magoli.

Kikosi cha Valverde kimepata ushindi wa sita mfululizo kwenye mechi za Primera Division ikimaanisha kuwa ni miongoni mwa timu nne pekee kwenye Ligi Kuu za Ulaya ambazo zimeweka rekodi hiyo sambamba na Juventus na Napoli za Italia na Porto ya Ureno.

Goli la Getafe lilileta mashaka ya pointi kwa Barca na miamba hao wa Catalan wakitokea nyuma waliifunga klabu hiyo yenye maskani yake Madrid, shukrani kwa magoli kutoka kwa Denis Suarez na Paulinho. Goli jingine pekee waliloruhusu klabu hiyo ya Catalan ni dhidi ya Eibar waliyoigaragaza 6-1 Camp Nou katikati ya juma.

 like facebook page yetu hapa kwa habari za uhakika Propellerads

For Booking>>>CALL>>>

Voda: +255757441463

JIUNGE NAMI KUPITIA LINK HIZI
No comments:

Post a Comment