TETESI ZA USAJIRI ZA MUDA HUU KUTOKA KONA YA DUNIA; HARZAD MBIONI KUTOKA CHELSEA - EDUSPORTSTZ | Habari za Ajira, Mapenzi, Michezo, Elimu, Kilimo, Technology, Siasa na Mziki,

BREAKING

Search here

TUFOLLOW UWE MIONGONI MWA WANAOTUMIWA HABARI KILA SIKU

Wednesday, 9 August 2017

TETESI ZA USAJIRI ZA MUDA HUU KUTOKA KONA YA DUNIA; HARZAD MBIONI KUTOKA CHELSEA

Eden Hazard
Eden Hazard yuko tayari kuondoka Chelsea na kujiunga na Real Madrid. (Don Balon)
Kylian Mbappe (kulia)

Paris Saint-Germain wapo tayari kupanda dau kumtaka mshambuliaji wa Monaco, Kylian Mbappe, 18, na wanajiandaa kutoa pauni milioni 161 kumtaka mchezaji huyo anayesakwa pia na Real Madrid na Manchester City. PSG watamuuza Angel Di Maria ili kupata fedha zaidi za kukamilisha usajili huo. (Le Parisien)

Liverpool watapanda dau la pauni milioni 60 kumtaka Virgil van Dijk kufuatia hatua ya mchezaji huyo kuwasilisha rasmi maombi ya kutaka kuondoka Southampton. Chelsea pia wanamtaka beki huyo, ingawa Antonio Conte anataka zaidi kusajili mabeki wa pembeni huku Serge Aurier wa PSG akiwa miongoni mwao. (Express)
Jose Mourinho

Meneja wa Manchester United Jose Mourinho ameghadhibishwa na matatizo ya beki wa PSG Serge Aurier ya kupata kibali cha kufanya kazi Uingereza, na hivyo kuamua kuelekeza nguvu zake kumtaka Fabinho wa Monaco na anadhani dau la pauni milioni 45 litatosha kumshawishi. (Don Balon)

Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp atakataa mkataba wowote kuhusu Philippe Coutinho kuondoka Anfield kwenda Barcelona. (Daily Mirror)

Liverpool hawataweza kumzuia Philippe Coutinho, 25, kuondoka msimu huu amesema mkongwe wa klabu hiyo Greame Souness. (Sky Sports)Philippe Coutinho

Mshambuliaji wa zamani wa kimataifa wa England Ian Wright amesema Philippe Coutinho "hana budi kwenda" Barcelona. (BBC Radio 5 Live)

Barcelona bado wanataka kumsajili mshambuliaji wa Borussia Dortmund Ousmane Dembele, 20. (Sport)

Manchester United watapanda dau kutaka kumsajili mshambuliaji wa Real Madrid Gareth Bale, 28, ikiwa mchezaji huyo ataachwa na Zinedine Zidane katika kikosi kitakachocheza fainali ya Uefa Super Cup. (Times)Zinedine Zidane

Meneja wa Real Madrid Zinedine Zidane ametupilia mbali taarifa za Gareth Bale kurejea England. (Mirror)

Chelsea na Manchester United zote zitapanda dau kumtaka beki wa PSG Serge Aurier, 24. (Daily Mail)

Kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater anajiandaa kuiambia klabu yake kuwa anataka kuondoka na kujiunga na Chelsea. (Mirror)

Chelsea wana matumaini makubwa ya kumpata beki wa Southampton Virgil van Dijk kwa sababu ya uhusiano tete kati ya Liverpool na Southampton. (Telegraph)

Southampton wanapanga kumsajili beki wa kati wa Middlesbrough Ben Gibson, 24, kuziba nafasi ya Virgil van Dijk. (Sun)

Mshambuliaji wa zamani wa Arsenal, Ian Wright amesema Arsenal walitakiwa kumsajili Nemanja Matic kutoka Chelsea kwa sababu timu hiyo inakosa kiongozi uwanjani. (BBC Radio 5 Live)

Manchester United na Inter Milan zimerejea tena kumtaka beki wa kushoto wa Tottenham Danny Rose, 27. (Daily Mirror)

Manchester City wamemuulizia kiungo wa Barcelona Sergio Busquets. (Onda Cero)Sergio Busquets

Valencia wanajiandaa kupanda dau la kumshawishi beki wa Arsenal Gabriel, 26, kuhamia Uhispania. (Evening Standard)

Trabzonspor ya Uturuki inataka kumsajili kiungo wa Tottenham Moussa Sissoko, 27, kwa mkopo. (Evening Standard)

No comments:

Post a Comment