STORI KUU ZA SOKA SIKU YA LEO - EDUSPORTSTZ

Latest

STORI KUU ZA SOKA SIKU YA LEO


Bale aliwasaidia Madrid kushinda Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya na taji la La Liga chini ya Zinedine Zidane msimu uliopita

Manchester United wamepewa matumaini na Real Madrid ya kumsajili Gareth Bale, 28. (Marca)

Manchester United watampa mkataba mpya beki wa kushoto Luke Shaw, 22, ili kuepuka asiondoke bure mwisho wa mkataba wake. (Sun)

Chelsea wanakaribia kumsajili kiungo wa Leicester City Danny Drinkwater, 27, kwa pauni milioni 40 pamoja na Alex Oxlade-Chamberlain, 24 kutoka Arsenal. (Express)

Chelsea wanakaribia kumuuza mshambuliaji wake Diego Costa, 28, kwenda Atletico Madrid kwa pauni milioni 30. (Mirror)

Liverpool bado wanamtaka beki Virgil van Dijk, 26. (Mail)

Liverpool wamethibitisha kufikia makubaliano ya kumsajili Naby Keita kutoka Red Bull Leipzig ifikapo Julai mosi 2018. (Sky Sports)

Liverpool wapo tayari kutumia pauni milioni 135 kuwasajili Virgil van Dijk na Thomas Lemar, baada ya kukamilisha usajili wa Naby Keita. (The Sun)Virgil van Dijk amechezea Uholanzi mechi 12

Mateo Kovacic ameonesha nia ya kutaka kujiunga na Liverpool na kuondoka Real Madrid. (Diario Gol)

Monaco wamekataa dau la pili kutoka Liverpool la kumtaka Thomas Lemar. (Sky Sports)

Swansea wanataka kumsajili kiungo wa Bayern Munich Renato Sanchez, 20. (Wales Online)

Manchester City wanapanga kupanda dau jingine kumtaka mshambuliaji wa Arsenal Alexis Sanchez, 28. (Goal)

Manchester City wanapanga kupanda dau jipya kumtaka beki wa kati wa West Brom Jonny Evans, 29, baada ya dau la pauni milioni 21 kutoka kwa Leicester kukataliwa. (Mirror)

Beki wa Manchester City Eliaquim Mangala, 26, huenda akajiunga na West Brom kama sehemu ya mkataba wa kumsajili Jonny Evans. (ESPN)

Meneja wa West Brom Tony Pulis anarejea Emirates na dau la pauni milioni 13 kumtaka beki Kieran Gibbs. (The Sun)


Tottenham huenda wakamkosa beki wa PSG Serge Aurier, 24, ambaye anataka kwenda Manchester United. (SFR Sport)

Sam Allardyce huenda akarejea Crystal Palace iwapo Frank de Boer atafukuzwa kazi. (Mirror)

Daktari wa timu ya taifa ya Brazil Michael Simoni amesema tatizo la mgongo la kiungo wa Liverpool Philippe Coutinho linasababishwa na msongo wa mawazo kuhusiana na hatma yake. (Sun)

Mkuu wa Juventus Beppe Marotta amesema klabu yake itapanda dau jipya kumtaka kiungo wa Liverpool Emre Can, 23, mwezi Januari. (Premium Sport)

Pepe Reina atabakia Napoli licha ya kupata nafasi ya kujiunga na Paris Saint-Germain. (AS)

Mkurugenzi wa Barcelona Robert Fernandez amesema klabu yake itasajili mchezaji mmoja au wawili zaidi kabla ya dirisha la usajili kufungwa, hii ni baada ya kukamilisha usajili wa Ousmane Dembele kwa pauni milioni 135. (Mundo Deportivo)

Juventus wanakaribia kukamilisha usajili wa Benedikt Howedes, 29, kutoka Schalke. (Gazzetta dello Sport)


Download our APP from Google Playstore using the link here>>>

Join Our Telegram Channel for Daily Updates CLICK HERE

No comments:

Post a Comment

Edusportstz